Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Shirka la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch, limetuhumu serikali za pembe ya Afrika kwa kushindwa kulinda haki za raia wake.
Kupitia taarifa yake ya kila Mwaka Human Rights watch, limesema mataifa mengi ya Pembe na Afrika yameshindwa kuzuia raia wake dhidi ya migogoro ya kivita ambayo imekuwa ikishuhudiwa kati ya wanajeshi wa serikali na makundi ya waasi.
Human Rights Watch pia imezituhumu serikali za Afrika kwa kuwadhulumu wanaharakati na wakosowaji wa serikali.

Mkurugezi mkuu wa Human Rights Watch Tirana Hassan, amesema kwamba serikali nyingi za Afrika zimeshindwa kujizuia kupokea maoni ya wapinzani wao na hivyo baadhi kama nchini Kenya, zimekuwa zikiwakamata na hata kuwaua wakosowaji wa serikali.
Nchini Sudan kwa mujibu wa mkurugezi wa Human Rights Watch kanda ya Afrika, Mausi Segun, jeshi na wapiganaji wa RSF wamekuwa wakiwalenga raia kwa risasi na kuharibu miundo mbinu kimakusudi.
Mausi ameongeza kuwa zaidi ya watu Milioni 12 wamekimbia makazi yao nchini Sudan kutokana na vita vinavyoendelea kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF.
Ripoti hiyo pia imeongeza kuwa pande hasimu nchini Ethiopia na Somalia, zilizuia misaada kuwafikia waathiriwa wa vita,huku maafisa wa kutoa huduma za misaada pia wakishambuliwa na hata kuuawa.
Aidha ripoti hiyo pia imeangazia vitendo vya utekaji ambavyo vinaendelea kuripotiwa nchini Kenya, hasa baada ya mswaada wa fedha wa mwaka 2024 kukataliwa na wandaamanaji.

Nchini Eritrea, Human Rights Watch imetuhumu serikali kwa kuwalazimisha raia wake kujisajili kufanya kazi kwa muda mrefu, mbali na kuwasaka raia wanakosowaji wake wanaoishi nje ya nchi na kuwakamata.
Kadhalika ripoti ya Human Right Watch imekosoa hatua ya serikali ya Sudan kusini kwa kuhairisha uchaguzi uliokuwa umeratibiwa kufanyika mwaka uliopita, hili likitajwa kuwa ukiukaji mkubwa wa raia kuwachagua viongozi wao
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.