Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mwanamke mmoja Mfaransa alilaghaiwa $850,000 na wanaojifanya mwigizaji Brad Pitt kwa usaidizi wa akili mnemba.
Kisa hicho kilitangazwa na kituo cha televisheni cha Ufaransa cha TF1, ambacho kiliamua kuondoa kipindi kumhusu mwanake huyo kutokana na wimbi la kejeli zilizotolewa dhidi ya yake.
Kipindi hicho kinachopeperushwa wakati wasikilizaji wengi wanasikiliza siku ya Jumapili, kilifanya wengi wao kuvutiwa na mwanamke huyo ambaye ni mbunifu na mpambaji wa majumba Anne, 53, ambaye alidhani alikuwa kwenye uhusiano na Pitt kwa mwaka mmoja na nusu.
Katika kipindi maarufu cha YouTube cha Ufaransa, Anne baadaye alisema yeye “sio kichaa wala mjinga”: “Nilidanganywa tu, nakubali na ndiyo maana nimejitokeza, kwa sababu sio mimi peke yangu.”
Mwakilishi wa Pitt aliiambia Entertainment Weekly kwamba “ilikuwa kitu kibaya kwamba matapeli huchukua fursa ya uhusiano mzuri wa mashabiki na watu mashuhuri” na kwamba watu hawapaswi kujibu mawasiliano ya mtu usiyemfahamu, “haswa kutoka kwa waigizaji ambao hawapo kwenye mitandao ya kijamii.
Mamia ya watumiaji mitandao walimdhihaki Anne, ambaye alikuwa amepoteza akiba yake na alijaribu kujitoa uhai mara tatu tangu ulaghai huo ulipotokea, kipindi cha televisheni kilisema.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.