Biden aonya juu ya utawala wa “wachache” katika hotuba yake ya kuaga watu kabla ya Trump kuapishwa.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

,

Rais anayemaliza muda wake wa Marekani Joe Biden ameonya juu ya utawala wa “wachache” unaojitokeza Marekani, alipokuwa akitoa hotuba yake ya kuaga na kumaliza taaluma yake ya miongo mingi katika siasa.

“Leo, utawala wa wachache umeanza kujitokeza katika Marekani ya utajiri mkubwa, nguvu na ushawishi ambao unatishia demokrasia yetu yote, haki zetu za msingi na uhuru,” alisema Jumatano.

Biden, mwenye umri wa miaka 82, alilenga wenye utajiri mkubwa “kijamii na kiuchumi” na kusema kunaweza kuwa na nguvu ya ajabu isiyodhibitiwa yenye kuwashinda Wamarekani.

Pia alitumia hotuba yake ya mwisho iliyopeperushwa moja kwa moja kutoka Ikulu ya White House kutoa maonyo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na upotoshaji wa mitandao ya kijamii.

Akizungumza kutoka Ikulu ambapo familia yake ilikuwa imekusanyika kutazama, aliangazia rekodi yake ya utawala wa muhula mmoja, akirejelea utengenezaji wa fursa za ajira, matumizi ya miundombinu, huduma ya afya, kuongoza nchi kutoka katika janga la corona, na kuifanya Marekani kuwa nchi salama.

Aliongeza, hata hivyo, kwamba “itachukua muda kuona matokeo kamili ya yote ambayo tumefanya pamoja, lakini mbegu zimepandwa, zitakua, zitachipuza na kuchanua kwa miongo kadhaa ijayo”.

Biden alitakia mafanikio utawala unaokuja wa Donald Trump, lakini akatoa maonyo kadhaa, huku rais akisema “mengi yako hatarini hivi sasa”.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment