Baraza la mawaziri la Israel kuidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Taarifa tunazoendelea kuzipa kipaumbele ni za Hamas na Israeli kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka baada ya miezi 15 ya vita.

Rais wa Marekani Joe Biden alipongeza hatua hiyo, akisema “utasitisha mapigano huko Gaza, na kuongeza msaada wa kibinadamu unaohitajika kwa raia wa Palestina, na kuwaunganisha mateka na familia zao”.

Baraza la Mawaziri la Israel linatazamiwa kukutana baadaye leo ili kuidhinisha makubaliano hayo, huku makubaliano ya awali ya wiki sita yakitarajiwa kuanza Jumapili hii.

Wapalestina wengi na familia za mateka wa Israel zimesherehekea habari hizo.

Shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza linasema kuwa takriban Wapalestina 20 wameuawa tangu makubaliano hayo yalipotangazwa jana jioni.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment