Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mwanamke mwenye ushawishi mkubwa nchini Australia ameshtakiwa kwa kumtilia sumu mtoto wake wa kike ili kuchangisha pesa na kuongeza wafuasi mtandaoni.
Mwanamke huyo wa Queensland alidai kwamba alikuwa na wakati mgumu kukabiliana na ugonjwa mbaya wa mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii, lakini wapelelezi wanadai kuwa alikuwa akimpa dawa za kulevya mtoto huyo wa mwaka mmoja na kisha kumrekodi akiwa katika hali ya “dhiki na maumivu makali”.
Madaktari walipaza sauti mnamo mwezi Oktoba, wakati mtoto alilazwa hospitalini akiwa mgonjwa sana.
Baada ya uchunguzi wa miezi kadhaa, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34 alishtakiwa kwa kumtesa mtoto, kumpa sumu, kumtumia mtoto vibaya nak wa ulaghai.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.