Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais mteule Donald Trump angehukumiwa kwa kujaribu kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2020 – ambayo alishindwa – ikiwa hangefanikiwa kuchaguliwa tena mwaka wa 2024, kulingana na ripoti ya Idara ya Sheria iliyotolewa kwa Bunge.
“Ushahidi unaokubalika ulitosha kumfungulia mashtaka,” ripoti ya Wakili Maalum Jack Smith ilisema.
Smith “amechanganyikiwa” na matokeo yake ni “feki”, Trump amejibu baada ya ripoti hiyo kutolewa.
Nyaraka hiyo ya kurasa 137 ilitumwa kwa Bunge baada ya Jaji Aileen Cannon kuruhusu kutolewa kwa sehemu ya kwanza kati ya mbili za ripoti ya Smith – kuhusu kesi ya kuingiliwa kwa uchaguzi.
Aliamuru kusikilizwa kwa kesi nyingine baadaye wiki hii kuhusu kutolewa kwa sehemu ya ripoti juu ya madai kwamba Trump alihifadhi hati za serikali kinyume cha sheria.
Rais mteule atachukua madaraka tarehe 20 Januari.
Wakili maalum, Jack Smith, alijiuzulu kutoka wadhifa wake wiki iliyopita.
Smith aliteuliwa mnamo 2022 kusimamia uchunguzi wa Idara ya Sheria ya Marekani juu ya Trump.
Mawakili maalum huchaguliwa na idara katika kesi ambapo kuna uwezekano wa mgongano wa maslahi.
Trump alishtakiwa kwa kuhifadhi hati kinyume cha sheria na, katika baadhi ya kesi, kuzihifadhi katika vyumba vya mapumziko ya Mar-a-Lago huko Florida, makazi yake ambayo anamiliki.
Katika kesi ya uingiliaji kati uchaguzi, alishtakiwa kwa kula njama ya kutengua matokeo ya uchaguzi wa 2020.
Kesi zote mbili zilisababisha mashtaka ya jinai dhidi ya Trump, ambaye alikanusha kuwa na hatia na kudai kuwa yaliyochochewa kisiasa.
Lakini Smith alifunga kesi hizo baada ya Trump kushinda uchaguzi mnamo mwezi Novemba, kwa mujibu wa kanuni za Idara ya Sheria zinazokataza kufunguliwa mashitaka kwa rais aliye madarakani.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.