Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani aitembelea Korea Kusini kwa mara ya kwanza baada ya miaka sita

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Takeshi Iwaya atakutana na mwenzake Cho Tae-yul nchini Korea Kusini Jumatatu, Januari 13, kulingana na Seoul, katikati ya machafuko ya kisiasa kwa jirani yake muhimu Korea Kusini na wiki moja kabla ya kurejea kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House.

Waziri wa Mambo ya Nje Takeshi Iwaya Novemba 11, 2024, Tokyo.
Waziri wa Mambo ya Nje Takeshi Iwaya Novemba 11, 2024, Tokyo. © Shuji Kajiyama / AP

Hii ni ziara ya kwanza kwa waziri wa mambo ya nje wa Japani nchini Korea Kusini kwa zaidi ya miaka sita, kulingana na shirika la habari la Yonhap, lililonukuliwa na shirika la habari la AFP.

Mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Cho Tae-yul na mwenzake wa Japani, Takeshi Iwaya, yatafanyika wakati Seoul ikitaka kuwahakikishia washirika wa kigeni kuhusu ahadi zake za kidiplomasia huku nchi hiyo ikikabiliwa na misukosuko kufuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Yoon Suk – Yeol na Bunge la taifa kwa jaribio lake lililoshindwa la kuweka sheria ya kijeshi mnamo Desemba 3.

Cho na Iwaya watakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu tukio lililoitumbukiza Korea Kusini katika mgogoro wa kisiasa. Mkutano na waandishi wa habari utafanyika baada ya mazungumzo yao kulingana na shirika la habari la Yonhap. Kabla ya mkutano huo, waziri wa Japan atatembelea makaburi ya kitaifa huko Seoul. Kesho, anatarajiwa atafanya ziara ya heshima kwa kaimu Rais Choi Sang-mok.

Ziara ya siku mbili ya Iwaya mjini Seoul ni ya kwanza kufanywa na mwanadiplomasia mkuu wa Japani kwa miaka saba. Mazungumzo ya leo yanatarajiwa kuangazia njia za kudumisha ushirikiano wa pande tatu na Marekani huku Trump, anayejulikana kwa kusitasita kukumbatia pande nyingi, ataapishwa kuwa rais Januari 20.

Mkutano wa Utatu wa Camp David wa Agosti 2023 uliwaleta pamoja viongozi kutoka nchi hizo tatu. Lakini rais wa Marekani na waziri mkuu wa Japani ni wapya. Na Korea Kusini kwa sasa inaongozwa na rais wa mpito.

Wakati huo huo, Cho na Iwaya wanatarajiwa kujadili matayarisho ya maadhimisho ya miaka 60 ya kuhalalisha uhusiano wa nchi hizo mbili mwaka huu, licha ya hali ya kisiasa nchini Korea Kusini. Wanaweza pia kujadili mpangilio wa mkutano wa kilele wa pande tatu na China ambao Japan itakuwa mwenyeji baadaye mwaka huu.

Ziara ya Iwaya mjini Seoul inafuatia ile iliyofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken wiki iliyopita. Tokyo, kama Washington, imeonyesha imani kwa Korea Kusini na utaratibu wake wa kidemokrasia.

Mkutano wa mwisho wa ana kwa ana kati ya Cho na Iwaya ulifanyika kando ya kongamano la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) nchini Peru Novemba mwaka jana. Waziri huyo wa Japani yuko katika ziara ya siku nne wiki hii ambayo pia itampeleka Ufilipino na Palau.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment