Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Korea Kaskazini inawahimiza wanajeshi wake waliotumwa Urusi kupigana dhidi ya Ukraine kujiua ili kuepusha kukamatwa, mbunge wa Korea Kusini amesema leo Jumatatu Januari 13, akinukuu idara ya ujasusi ya Seoul.

“Maelezo yaliyopatikana kwa wanajeshi waliofariki yanaonyesha kwamba mamlaka ya Korea Kaskazini iliwashinikiza kujiua,” ikiwa ni pamoja na “kujilipua (…) kabla ya kukamatwa,” Lee Seong-kweun amewaambia waandishi wa habari, akinukuu taarifa kutoka kwa idara ya ujasusi ya Korea Kusini.
“Makadirio yanaonyesha kuwa idadi ya waliopoteza maisha kati ya vikosi vya Korea Kaskazini imezidi 3,000, ikiwa ni pamoja na takriban 300 waliofariki na 2,700 kujeruhiwa,” Lee Seong-kweun amewaambia waandishi wa habari baada ya taarifa ya kijasusi ya Korea Kusini, shirika la habari la AFP limeripoti.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.