‘Niko tayari kwa mabadilishano ya wanajeshi wa Korea Kaskazini’ – Zelensky

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema yuko tayari kuwakabidhi wanajeshi wawili waliokamatwa kutoka Korea Kaskazini kurudi katika nchi yao ili kubadilishana na wafungwa wa kivita wa Ukraine nchini Urusi.

“Kwa wale wanajeshi wa Korea Kaskazini ambao hawataki kurejea, kunaweza kuwa na machaguo mengine,” Zelensky alisema kwenye mtandao wa kijamii, na kuongeza “wale wanaoonyesha nia ya kuleta amani kwa kueneza ukweli juu ya vita hivi nchini Korea, watapewa fursa hiyo”.

Ukraine ilisema Jumamosi kwamba watu hao walikamatwa tarehe 9 Januari.

Alipoulizwa mwaka jana, Rais Vladmir Putin hakukanusha kuwa Urusi ilikuwa ikitumia wanajeshi wa Korea Kaskazini katika vita vyake dhidi ya Ukraine, akisema huo ni uamuzi wa Urusi.

Huduma ya Usalama ya Ukraine ilisema wanajeshi hao wawili wako Kyiv na wanapokea matibabu.

Wanazungumza Kikorea pekee na wanahojiwa kwa usaidizi wa (Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi) nchini Korea Kusini, idara ya ujasusi ilisema.

Zelensky alichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii Jumamosi zikiwaonyesha wanaume hao, ambao wamejeruhiwa.

Ofisi ya Zelensky ilisema katika taarifa yake Jumamosi kwamba Warusi “wanajaribu kuficha ukweli kuwa hawa ni wanajeshi kutoka Korea Kaskazini kwa kuwapa hati zinazodai wanatoka Tuva au maeneo mengine chini ya udhibiti wa Moscow”.

Habari za BBC na vyombo vingine vya habari vya kimataifa bado havijathibitisha madai ya Ukraine ya wafungwa na kukamatwa kwao.

Ukraine na Korea Kusini ziliripoti mwishoni mwa mwaka jana kwamba Korea Kaskazini ilituma takriban wanajeshi 10,000 nchini Urusi.

Ikulu ya White House ilisema kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini ndio wenye kuathirika kwa kupata majeraha makubwa.

Mnamo mwezi Desemba, shirika la ujasusi la Korea Kusini liliripoti kwamba mwanajeshi wa Korea Kaskazini anayeaminika kuwa wa kwanza kukamatwa akiunga mkono vita vya Urusi nchini Ukraine alikufa baada ya kuchukuliwa akiwa hai na vikosi vya Ukraine.

Zelensky alisema Jumapili “hapana shaka kwamba jeshi la Urusi linategemea msaada wa kijeshi kutoka Korea Kaskazini.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment