Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Takriban raia 16 katika Jimbo la Zamfara kaskazini-magharibi mwa Nigeria wameuawa katika shambulio la anga la kijeshi, baada ya kudhaniwa kuwa ni magenge ya wahalifu.
Wakazi waliambia vyombo vya habari vya ndani kuwa wahasiriwa walikuwa wanachama wa vikundi vya walinzi wa eneo hilo na raia wanaojilinda dhidi ya magenge yenye silaha yanayowateka watu kwa lengo la kupata kikombozi.
Mashambulizi hayo yalilenga magenge ya wanamgambo katika maeneo ya Zurmi na Maradun na gavana wa jimbo hilo, Dauda Lawal, alitoa rambirambi zake kwa jamii.
Jeshi limekiri kufanya mashambulizi ya angani, ambayo ilisema ni “pigo kubwa kwa majambazi wanaovamia vijiji katika eneo hilo”.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.