Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Guinea, serikali imesitisha vyama vya siasa ambavyo havidhaidhinishwa, matokeo ya kampeni ya tathmini ya vyama vyote vya nchi hiyo iliyofanywa mwezi Oktoba mwaka uliyopita. Haya yanatakiwa kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwezi wa Januari, ili kujiandaa kwa uchaguzi ujao mwaka huu, kama rais wa mpito Mamadi Doumbouya alivyoahidi wakati wa hotuba yake ya kuwatakiwa raia wake Heri ya Mwaka Mpya.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Utawala ya Guinea inachukizwa na kuenea kwa vyama ambavyo hajaidhinishwa na utawala na inadai kukomesha shughuli za vyama hivyo. Akirejelea matokeo ya tathmini ya vyama vya siasa mwaka jana, Waziri Ibrahima Kalil Condé anakaribisha taasisi zote na washirika kusitisha ushirikiano wao na vyama 54 vilivyositishwa. Vyama hivi vilikuwa na miezi 3 ya kukamilisha taratibu zote zinazoidhinishwa na sheria, uda wa mwisho ni Januari 2025.
Uamuzi huu unakuja siku 10 baada ya hotuba ya Jenerali Mamady Doumbouya kuwatakiwa raia wake Heri ya Mwaka Mpya. Rais huyo wa mpito alitangaza kuwa mwaka 2025 utakuwa mwaka muhimu wa uchaguzi kwa ajili ya kurejea kwa utaratibu wa kikatiba, na kwamba hivi karibuni atatangaza tarehe ya kura ya maoni na kwamba vyama vya siasa vinaweza kuanzisha tena shughuli zao kikamilifu.
Mnamo Januari 9, 2025, , msemaji wa serikali Ousmane Gaoual Diallo alibainisha kuwa kura ya maoni inaweza kufanyika mnamo mwezi Mei.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.