Gaza: Idadi ya vifo yakadiriwa kufikia 41%, kulingana na utafiti uliochapishwa The Lancet

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Utafiti uliochapishwa siku ya Alhamisi, Januari 9, katika Jarida maarufu la matibabu la Uingereza la The Lancet inakadiria kwamba idadi ya vifo huko Gaza, wakati wa miezi tisa ya kwanza ya vita kati ya Israeli na Hamas, ni zaidi ya 41% kuliko ile iliyorekodiwa na wizara ya afya ya Hamas. 

Miili ya Wapalestina baada ya mashambulizi ya Israel huko Gaza, Januari 2, 2024.
Miili ya Wapalestina baada ya mashambulizi ya Israel huko Gaza, Januari 2, 2024. AP – Mohammed Hajjar

Idadi ya watu waliouawa huko Gaza imezua mjadala mkali tangu Israel ilipoanzisha kampeni yake dhidi ya Hamas kujibu mashambulizi katika eneo lake Oktoba 7, 2023. Tangu kuanza kwa vita hadi Juni 30 mwaka jana, Wizara ya Afya ya Hamas iliripoti idadi ya vifo 37,877.

Utafiti wa Jarida la The Lancet, hata hivyo, unakadiria kuwa kati ya vifo 55,298 na 78,525 vilisababishwa na majeraha huko Gaza katika kipindi hiki. Idadi ya vifo vilivyobainishwa na Jarida la Lancet ni vifo 64,260 hadi sasa, zaidi ya 41% kuliko makadirio ya Wizara ya Afya ya Hamas. Idadi hiyo inawakilisha asilimia 2.9 ya wakazi wa Gaza kabla ya vita, “au takriban mmoja kati ya wakazi 35,” kulingana na utafiti huo.

Idadi hii inahusu tu vifo vinavyotokana na majeraha ya kiwewe na kwa hivyo haijumuishi vifo visivyo vya moja kwa moja, kama vile kukosa matunzo au chakula, wala maelfu ya watu waliopotea wanaofikiriwa kufukiwa chini ya vifusi.

Siku ya Alhamisi, Januari 9, wizara ya afya ya Hamas ilisema kuwa watu 46,006 walikufa wakati wa vita vya miezi kumi na tano, wengi wao wakiwa waliuawa katika mashambulizi ya mabomu ya Israeli. Huko Israeli, mashambulizi ya umwagaji damu yaliyofanywa na Hamas mnamo Oktoba 7, 2023 yalisababisha vifo vya watu 1,208, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP ikijikita takwimu rasmi za Israeli.

Israel imetilia shaka uaminifu wa takwimu za wizara ya afya ya Hamas, lakini zimeonekana kuwa za kuaminika na Umoja wa Mataifa.

Kutumia njia ya takwimu inayoitwa “capture-recapture”

Watafiti katika utafiti huo uliochapishwa na The Lancet walitumia mbinu ya takwimu iitwayo “capture-recapture” ambayo imetumika kukadiria idadi ya vifo katika migogoro mingine duniani – kwa mfano Kosovo na Guatemala – ambayo inajikita kwa orodha tatu. 

orodha ya kwanza ni ile iliyotolewa na Wizara ya Afya na inajumuisha miili inayotambuliwa katika hospitali au vyumba vya kuhifadhia maiti. Orodha ya pili inatoka kwenye uchunguzi wa mtandaoni uliozinduliwa na Wizara ya Afya, ambapo Wapalestina waliripoti vifo vya jamaa zao. Orodha ya tatu ilianzishwa kutoka kwa kumbukumbu zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii kama X, Instagram, Facebook na Whatsapp, wakati utambulisho wa waliofariki uliweza kuthibitishwa.

“Tumejumuisha tu katika utafiti wetu watu ambao vifo vyao vilithibitishwa na jamaa zao au na vyumba vya kuhifadhia maiti na hospitali,” Zeina Jamaluddine, mtaalam wa magonjwa katika chuo chaLondon School of Hygiene and Tropical Medicine, ameliambia shirika la habari la AFP.

Watafiti kisha wakachunguza orodha za vifo kwa nakala. “Tulitafuta mwingiliano kati ya orodha tatu (…) ili kupata makadirio ya jumla ya watu waliouawa,” amesema Zeina Jamaluddine.

Utafiti hauzingatii watu waliotoweka

Waandishi wa utafiti huo wamehimiza tahadhari, wakielezea kuwa orodha zilizochapishwa na hospitali hazionyeshi sababu ya vifo kila wakati, kwa hivyo inawezekana kwamba watu walio na hali ya kiafya isiyo ya kiwewe, kama vile mshtuko wa moyo, walijumuishwa, hali ambayo inaweza kusababisha kukadiria kupita kiasi.

Kuna, hata hivyo, sababu nyingine kwa nini mateso ya vita vya Gaza yanaweza kukadiiwa kwa idadi ndogo. Utafiti haukuzingatia watu waliotoweka. Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu OCHA limesema takriban watu 10,000 kutoka Gaza waliotoweka, wanaaminika kuzikwa chini ya vifusi.

Zeina Jamaluddine amekiri kwamba alitarajia “ukosoaji kutoka pande zote” kuhusu utafiti huu. Amezungumza dhidi ya kile alichokiita “uchungu” wa takwimu za vifo: “Tunajua kwamba idadi ya vifo iko juu sana,” amesema.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment