Gabon: Wabunge wa mpito wachunguza rasimu kubwa ya sheria kuhusu kanuni mpya ya uchaguzi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini Gabon, wabunge wa mpito wanaitwa kwenye kikao kisicho cha kawaida kuanzia Januari 10, 2025, kwa siku kumi. Watachunguza rasimu ya sheria kuhusu kanuni mpya ya uchaguzi nchini. Rasimu hii iliandikwa na kundi la wataalam, walioteuliwa katikati ya mwezi wa Desemba na rais wa mpito, na wakiongozwa na Waziri wa Marekebisho ya Kitaasisi, Murielle Minkoué. Atasimia uchaguzi wa mwisho wa mpito uliopangwa kufanyika hivi karibuni mwezi wa Agosti mwaka huu.

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Gabon, Libreville, Septemba 7, 2023.
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Gabon, Libreville, Septemba 7, 2023. AFP – –

Mabadiliko ya mfumo wa kisheria yamepangwa, lakini muda mfupi unaotolewa kwa wabunge unazua maswali. 

Kuna Ibara 383 zinazojumuishwa katika vitabu vinne, vyenye vichwa 18 na sura 58, na siku 10 pekee za kuzijadili, kuziidhinisha au kuzirekebisha: tarehe hii fupi ya mwisho haishindwi kutoa changamoto kwa baadhi ya wabunge na maseneta nchini Gabon, ambao wanaogopa jukumu rahisi la ” kurekodi” mradi ambao hata hivyo ni “msingi” kwa ajili ya kuendeleza kipindi cha mpito kilichoanza kufuatia mapinduzi yaliyomng’oa mamlakani Ali Bongo Ondimba mnamo Agosti 30, 2023.

Katika kupitisha rasimu hiyo, serikali imeahidi kwamba itaruhusu uchaguzi “huru, wazi na wa kidemokrasia”. Uchaguzi huu utasimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, kama kura ya maoni ya katiba ya mwezi wa  Novemba 2024, ambayo upinzani ulikosoa vikali. Lakini mradi huo unatoa fursa ya kuundwa kwa tume maalumu na kuongeza mamlaka ya udhibiti – Mamlaka ya Kudhibiti na Kusimamia Uchaguzi na Kura za Maoni (ACSE) – inayoundwa na “watu wasio na upendeleo na wenye uwezo”. Taasisi ya usimamizi isiyo ya kudumu ambayo itaweza “kutoa mapendekezo ya kurekebisha au kuzuia kasoro zinazowezekana,” kulingana na serikali.

Mamlaka ya mpito imetetea mara kwa mara uwezo wa Wizara ya Mambo ya Ndani katika masuala ya uchaguzi, ikikumbusha kuwa tume ya zamani ya Uchaguzi nchini Gabon (CGE) haijawahi kuonyesha uhuru.

Hata hivyo, rasimu hii hutoa upendeleo wa lazima katika orodha za wagombea, yaani angalau 30% ya wanawake na 20% ya vijana. Pia inanuia “kuhakikisha upatikanaji sawa kwa wagombea kwenye vyombo vya habari vya umma”, kuweka na kudhibiti matumizi ya kampeni, na kuhakikisha kutegemewa kwa daftari la wapiga kura la kibayometriki.

Katika ratiba ya mpito, kanuni za uchaguzi zilipaswa kujadiliwa kuanzia mwezi wa Januari hadi katikati ya mwezi Machi, na orodha ya wapiga kura kufanyiwa marekebisho mwezi Aprili. Sasisho hili hatimaye lilianza Januari 2, 2025 na limeratibiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment