DR Congo: OCHA yaonya kuhusu kuzorota kwa hali mbaya ya kibinadamu Kivu Kaskazini

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na masuala ya kubinadamu OCHA, inaonya kuwa, hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya katika jimbo la Kivu Kaskazini, kunakoshuhudiwa vita kati ya jeshi la FARDC na waasi wa M 23.

Takriban watu 200,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano mapya katika maeneo ya Rutshuru na Masisi, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.
Takriban watu 200,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano mapya katika maeneo ya Rutshuru na Masisi, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA. © AFP

Mkuu wa tume hiyo Bruno Lemarquis, ametoa kauli hii, baada ya ripoti kuwa vita vinavyoendelea vimesbabisha watu zaidi ya 100,000 kuyakimbia makaazi yao ndani ya kipindi cha siku 10 zilizopita. OCHA inasema, watu hao wamekimbia makaazi yao tangu Januari tarehe 1 wakati vita, vilivyoanza katika wilaya ya Masisi.

Umoja wa Mataifa sasa unataka machafuko na mashambulio dhidi ya raia kukoma na wafanyakazi wa kutoa misaada kuruhusiwa kuwafikia watu wenye uhitaji wa chakula, maji na dawa.

Wakati hayo yakijiri, jeshi la serikali linaloshirikiana na wapiganaji wa Wazalendo, linasema, limewafanikiwa kudhibiti tena mji wa Ngungu, Kaskazini mwa Masisi uliokuwa umechukuliwa na waasi wa M23.

Msemaji wa jeshi Kivu Kaskazini, Luteni Kanali Guillaume Njike Kaiko, amesema maafisa wa usalama wanafanya kila linalowezekana, kuhakikisha kuwa wananchi wanaishi kwa amani.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment