Sarkozy aiambia mahakama ‘si japokea hata senti’ moja kutoka Libya katika fedha za kampeni

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, ameiambia Mahakama jijini Paris kuwa hakuwahi kupokea, hata senti moja, fedha haramu kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya Moamer Gadhafi, kumsaidia kufanya kampeni mwaka 2007.

Sarkozy atakuwa kizimbani katika mahakama mjini Paris chini ya nusu mwezi baada ya mahakama ya rufaa ya Ufaransa hapo Desemba 18 kukataa ombi lake la kisheria dhidi ya kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa ushawishi wa kibiashara, ambapo anatakiwa kuvaa kifaa maalum mkononi badala ya kwenda gerezani.
Sarkozy atakuwa kizimbani katika mahakama mjini Paris chini ya nusu mwezi baada ya mahakama ya rufaa ya Ufaransa hapo Desemba 18 kukataa ombi lake la kisheria dhidi ya kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa ushawishi wa kibiashara, ambapo anatakiwa kuvaa kifaa maalum mkononi badala ya kwenda gerezani. AFP – BERTRAND GUAY

Kesi dhidi ya Sarkozy, mwenye umri wa miaka 69, itaendelea hadi Aprili tarehe 10 na ikiwa atapatikana na kosa, atafungwa jela miaka 10.

Rais wa zamani wa UfaransaNicolas Sarkozy tayari amehukumiwa katika kesi mbili tofauti tangu alipoondoka madarakani.

Wadhifa wa Sarkozy umegubikwa na matatizo ya kisheria tangu aliposhindwa uchaguzi wa rais mwaka 2012. Lakini alibaki kuwa kiongozi maarufu kwa wengi wa mrengo wa kulia na pia anajulikana kukutana mara kwa mara na Rais Emmanuel Macron.

Mwanasiasa mwenye utashi mkubwa na nguvu, ana miaka 69, na mke wake ni mwana mitindo na muimbaji Carla Bruni, na wakati akiwa madarakani kutoka mwaka 2007 mpaka 2012 alipenda kujulikana kama “rais mwenye hamasa kubwa sana,” amehukumiwa katika kesi mbili, na kushtakiwa katika nyingine na anachunguzwa kuhusiana na nyingine mbili zaidi.

Sarkozy atakuwa kizimbani katika mahakama mjini Paris chini ya nusu mwezi baada ya mahakama ya rufaa ya Ufaransa hapo Desemba 18 kukataa ombi lake la kisheria dhidi ya kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa ushawishi wa kibiashara, ambapo anatakiwa kuvaa kifaa maalum mkononi badala ya kwenda gerezani.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment