Polisi wa Afrika Kusini wawaokoa wahamiaji 26 wakiwa watupu wameshikiliwa mateka

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

[ok
Maelezo ya picha,Polisi walitoa picha hii ya dirisha lililovunjwa ambalo baadhi ya waliopatikana walilitumia kutoroka

Polisi wa Afrika Kusini wamewaokoa wahamiaji 26 wanaoaminika kutoka Ethiopia, waliokuwa wamezuiliwa katika nyumba moja jijini Johannesburg.

Kumi na watano kati yao walipatikana wakiwa uchi huku wengine 11 – wakiwa na majeraha katika eneo la karibu.

Polisi wamesema uokoaji huo ulifanywa siku ya Alhamisi jioni katika kitongoji cha kaskazini-mashariki mwa jiji kufuatia taarifa kutoka kwa majirani.

Watu watatu wamekamatwa.

Haijabainika jinsi wahamiaji hao walivyofika Afrika Kusini, lakini serikali inachunguza iwapo walikuwa wahanga wa ulanguzi.

Maafisa hawajatoa maelezo kuhusu hali ambazo wahamiaji hao walikutwa nazo na kwa nini wengine walikuwa uchi.

Wale ambao walipatikana karibu na eneo hilo walikuwa wamevunja “dirisha na kutoroka,” kulingana na Kanali Philani Nkwalase, msemaji wa Hawks, shirika la polisi wanaoshughulikia uhalifu mkubwa.

Wale ambao walikuwa wamejeruhiwa wakati wakijaribu kukimbia walipelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Washukiwa watatu wanaoshikiliwa na polisi walipatikana na bunduki haramu na wanadaiwa kuhusika na ulanguzi wa binadamu.

Mwezi Agosti mwaka jana raia 90 wa Ethiopia wasio na hati walipatikana wameshikiliwa kinyume na matakwa yao na katika mazingira magumu katika nyumba moja mashariki mwa Johannesburg.

Polisi wa eneo hilo, katika operesheni iliyohusisha mashirika mengine, waliwapata watu hao wakati wakimtafuta mtu aliyetekwa nyara, ambaye pia alipatikana kwenye nyumba hiyo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment