Mashariki mwa DRC: Mapigano yarindima kusini mwa wilaya ya Lubero

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mapigano yameripotiwa tena kuanzia leo asubuhi, Kusini mwa Wilaya ya Lubero katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC kati ya wanajeshi wa serikali FARDC na waasi wa M 23 wanaoungwa mkono na Rwanda.

Wanajeshi wa FARDC katika eneo la Lubero (hapa ilikuwa mwezi Oktoba mwaka uliyopita), huko Kivu Kaskazini, ambako mapigano na waasi wa M23 yameanza tena kwa wiki moja.
Wanajeshi wa FARDC katika eneo la Lubero (hapa ilikuwa mwezi Oktoba mwaka uliyopita), huko Kivu Kaskazini, ambako mapigano na waasi wa M23 yameanza tena kwa wiki moja. © Djaffar Al Katanty / REUTERS

Maafisa wa ya usalama wamesema, vita hivyo vilizuka baada ya waasi wa M23 kuvamia vijiji  vya Kyulo na Timbo Timbo, vinavyodhibitiwa na jeshi, umbali wa Kilomita 50 kutoka mjini Lubero.

Mapigano hayo yamekuja baada ya kushuhudiwa kwa utulivu wa siku tatu, Kusini mwa Lubero, ambako waasi na wanajeshi wamekuwa wakikabiliana.

Wakati hayo yakijiri, msemaji wa jeshi ma DRC jimboni Kivu Kaskazini Guillaume Ndjike, amesema FARDC inaendelea na operesheni ya kuwarudisha nyuma waasi wa M23 wilayani Masisi.

Kauli yake imekuja, baada ya jeshi kuripoti kuwa, wameudhibiti tena mji wa Masisi ambao wiki iliyopita, ulikuwa mikononi mwa waasi wa M23.

Siku ya Alhamisi jeshi limepigana na waasi hao katika mji wa Ngungu, huku wengine wakiripotiwa kujificha katika mlima wa Kahongole, karibu na mji wa Masisi.

Katika hatua nyngine, katika mkoa jirani wa Ituri, shughuli za kawaida zimekwama katika mji wa Biakato, Wilayani Mambasa, baada ya wanaharakati kuitisha mgomo wa siku tatu kuanzia siku ya Alhamisi, kulalamikia utovu wa usalama katika eneo hilo

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment