Kutokuwepo kwa utulivu mashariki mwa Congo kumetokana na historia ya kikoloni – Kagame

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Maelezo ya picha,Rais wa Rwanda Paul Kagame

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesisitiza kuwa wapiganaji wa Kundi la M23 wanaozua ghasia nchini DR Congo hawafadhiliwi na serikali yake kama inavyodaiwa.

Rais Kagame alieleza kuwa vita katika eneo la mashariki mwa Kongo vimekuwa vikiendelea kwa miaka mingi, na kuuliza ‘’Je watu hapa hawajui jinsi vita hivi vilivyoanza? Vita hivi vilianza miaka mingi iliyopita na haikutokana na Rwanda.’’

Aliongeza kuwa ‘’Vita hivi vilianzishwa na makundi yalikuwepo Congo na huenda baadhi yao wana asili ya Rwanda lakini walikuwa wamehamia Congo tangu enzi za ukoloni’’

Rais Kagame amesema kuwa ingawa viongozi wa Congo wameonekana kukiri kuwa waasi hao ni Wakongo lakini cha kushangaza wanadai kuwa vita hivi vinaungwa mkono na Rwanda.

Kauli ya rais Kagame inajiri baada ya kuchukua udhibiti wa mji wa Masisi siku tatu zilizopita kundi la M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Rwanda inadaiwa kutumia kundi la M23 kupora madini kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kama vile dhahabu, cobalt na tantalum, ambayo hutumiwa kutengeneza simu za mkononi na betri za magari yanayotumia umeme.

Mwezi uliopita, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilisema inaishitaki Apple kwa matumizi yake ya “madini haramu,” na kuifanya kampuni hiyo kubwa ya teknolojia kusema kuwa imeacha kutumia madini kutoka kwa nchi hizo mbili.

Rwanda imekanusha kuwa mshirika wa usafirishaji wa madini haramu kutoka DR Congo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment