Wasiwasi watanda Msumbiji wakati kiongozi wa upinzani akirejea kutoka uhamishoni

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

d
Maelezo ya picha,Venâncio Mondlane anashikilia kuwa alishinda uchaguzi wa rais wa mwaka jana kwa madai kuwa kura ziliibiwa.

Kiongozi wa upinzani nchini Msumbiji aliye uhamishoni Venancio Mondlane amerejea nchini leo kabla ya kuapishwa kwa rais mpya wiki ijayo kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata.

Baada ya kutua Maputo, Mondlane amesema anarejea kuwa karibu na vuguvugu la maandamano, ambalo limefanya maandamano ya wiki kadhaa nchini kote na watu 300 wanaaminika kuuawa.

Mondlane anadai uchaguzi wa Novemba uliibiwa, madai yanayoungwa mkono na waangalizi huru.

Kabla ya kutua kwake, uwanja wa ndege ulikuwa na ulinzi mkali huku maafisa wa polisi wakijaribu kuwazuia wafuasi wa Mondlane kufika eneo hilo.

Barabara zinazoelekea katika uwanja huo wa ndege zilifungwa na vikosi vya usalama vikiwazuia watu kufika uwanja wa ndege isipokuwa wawe na tiketi ya ndege.

Mabomu ya machozi yalirushwa kwa umati wa watu katika eneo hilo na walenga shabaha waliwekwa kwenye majengo ya karibu, limeripoti shirika la habari la Reuters.

Matokeo rasmi ya mwisho kutoka mahakama ya katiba wiki mbili zilizopita yalimpa Daniel Chapo 65% ya kura na Mondlane 24%.

Tangu uchaguzi wa Oktoba, mawimbi ya maandamano yamesababisha zaidi ya watu 270 wakiwemo waandamanaji na wanachama wa vikosi vya usalama kuuawa, kulingana na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment