Ningemshinda Donald Trump katika uchaguzi wa urais- Joe Biden

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Biden

Rais wa Marekani Joe Biden amesema anaamini angeweza kumshinda Donald Trump na kuibuka mshindi ka uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana.

Akizungumza na gazeti la USA Today katika mahojiano ya kipekee, Biden amekiri kuwa umri wake ungemzuia kutekeleza majukumu ya urais iwapo angechaguliwa kwa muhula mwingine wa miaka minne.

“Hadi sasa, hali ni nzuri,” alisema Biden mwenye umri wa miaka 82. “Lakini nani anajua nitakuwa nani nikiwa na miaka 86?” Katika mahojiano hayo na Susan Page

Biden pia alisema kuna uwezekano wa kutoa msamaha kwa maadui wa Trump wakiwemo aliyekuwa mbunge wa chama cha Republican, Liz Cheney, na aliyekuwa mkurugenzi wa masuala ya afya, Dr. Anthony Fauci.

Akielezea walichokizungumzia katika mkutano wao na Trump uliofanyika katika Ofisi ya Rais baada ya uchaguzi wa Novemba alimshauri Trump hakuna haja ya Trump kurudi nyuma na kujaribu kulipiza kisasi.

“Nilijaribu kufafanua kwamba hakuwa na haja ya kufanya hivyo, na ilikuwa kinyume na maslahi yake kurudi nyuma na kulipiza kisasi,” Biden alisema, akiongeza kuwa Trump hakupinga, bali “aliguswa tu na kusikiliza.”

Rais Biden alisema uamuzi wake wa mwisho utategemea Trump atachagua nani katika baraza lake la mawaziri.

Katika mkutano huo huo, Biden alisema Trump alikuwa “akimpongeza” kuhusu rekodi yake ya uchumi. “Alifikiri kwamba ningeondoka na rekodi nzuri,” alisema Biden, ambaye ni mjumbe wa chama cha Democratic.

Mahojiano hayo na USA Today ndio mahojiano pekee ya kuaga aliyopewa na Biden kwa gazeti la uchapishaji.

Vile vile,rais Biden ametetea msamaha aliotoa kwa mwanawe, Hunter Biden, licha ya awali kusema hatafanya hivyo.

Biden, ambaye alifika bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1972 kama seneta wa Marekani, alikosolewa na chama chake mwenyewe kwa kuchelewa kujiondoa katika kinyang’anyiro cha urais ambapo makamu wake Kamala Harris alishindwa na Trump katika uchaguzi wa urais.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment