Mtoto azaliwa kwenye boti ya wahamiaji ilioelekea Visiwa vya Canary kutoka Afrika

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mtoto azaliwa kwa boti siku ya Jumatatu
Maelezo ya picha,Mtoto azaliwa kwa boti siku ya Jumatatu

Mtoto wa kiume amezaliwa kwenye boti ya wahamiaji iliyojaa watu, iliyosafiri kutoka Afrika hadi Visiwa vya Canary wiki hii.

Boti hiyo ilionekana kwa mara ya kwanza tarehe 6 Januari karibu na kisiwa cha Lanzarote. Walinzi wa pwani walifika baada ya mtoto kuzaliwa, siku ambayo Uhispania ilisherehekea sherehe za Epifania.

Nahodha wa boti ya uokoaji Domingo Trujillo amesema walijua kuwa kulikuwa na mwanamke mjamzito, lakini walishtuka walipokutana na mtoto aliyezaliwa dakika chache zilizopita.

Mama na mtoto walikimbizwa hospitalini kwa huduma za ziada za matibabu katika kisiwa cha Lanzarote. Hakukuwa na matatizo mengine yoyote yaliyoripotiwa na mamlaka.

Kamanda wa helikopta alielezea kuwa kuzaliwa kwa mtoto ilikuwa “zawadi bora zaidi” waliyopokea siku hiyo.

Safari ya kuvuka bahari kutoka Afrika hadi Visiwa vya Canary ni hatari sana, na mwaka jana zaidi ya wahamiaji 46,800 walifanya safari hii.

Epifania, sikukuu maarufu ya Kikristo, inasherehekewa sana Uhspania, ambapo watoto hupokea zawadi kutoka kwa Wafalme Watatu.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment