Marekani yatangaza msaada mpya wa dola milioni 500 kwa Ukraine

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

fdc
Maelezo ya picha,Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin

Marekani imetangaza msaada mpya kwa Kyiv wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 500, msaada wa mwisho kabla ya kuapishwa kwa Donald Trump.

Hayo yametangazwa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin katika kambi ya jeshi la Marekani ya “Ramstein” nchini Ujerumani, ambako mkutano wa nchi za Magharibi na Ukraine unafanyika.

Msaada huo unajumuisha makombora ya ulinzi wa anga ya Ukraine, makombora ya kushambulia na vifaa vingine vya kuzisaidia ndege za F-16 za Ukraine, imeripoti RBC-Ukraine.

Huu ni mkutano wa mwisho katika kambi ya Ramstein kabla ya rais mteule Donald Trump kuingia madarakani nchini Marekani.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment