DR Congo: Raia waandamana mjini Bukavu kutokana na ukosefu wa usalama Mashariki mwa nchi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini DRC, asasi za kiraia zimefanya maandamano hapo jana siku ya Jumatano mjini Bukavu kupinga vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi hiyo, lakini pia  kuonesha hasira dhidi ya uchimbaji madini kinyume cha sheria.

Waandamanaji wa wa DRC wakiingia katika mitaa ya Kinshasa na Bukavu wiki hii wakipinga madai ya Rwanda kuungwa mkono na waasi wa M23 wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC.
Waandamanaji wa wa DRC wakiingia katika mitaa ya Kinshasa na Bukavu wiki hii wakipinga madai ya Rwanda kuungwa mkono na waasi wa M23 wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC. © RadioStar

Akiwa anajifunika bendera ya Congo kichwani, Bwenda Ngalu Joseph ni mkazi wa Kijiji cha Nzovu katika wilaya ya Shabunda aliyeshiriki maandamano haya ili kuwasilisha madai yake.

«Nilipenda nishiriki maandamano sababu barabara yetu ya wilaya ya Shabunda inaharibika kufuatia uchimbaji dhahabu unaofanyika na wachina kwetu Shabunda»

Wakiwa na mabango kadhaa kulikoandikwa ujumbe wakutaka amani, waandamanajii walisisitiza hasa zaidi kuhusu uchimbaji madini unaofanyika kiholela katika jimbo la Kivu kusini. Néné Bintu ni msimamizi wa ofisi ya uratibu wa asasi za kiraia mjini Bukavu aliyeongoza maandaman hayo.

«Tunataka Rais wa Jamhuri achunguze kinachofanyika katika jimbo letu sababu kuna hata habari zinazosema kwamba hata familia yake inahusika katika uchimbaji madini. Asinyamaze»

Haya yayajiri kufuatia kukamatwa kwa wachina 3 jumamosi iliopita wakiwa na vifurushi vingi vya dhahabu na kiwango kikubwa cha pesa. Kwasasa serikali ya Kinshasa inataka vipelekwe mjin Kinshasa. Gavana wa Kivu kusini profesa alionya wakazi kuwa waangalifu akiwahakikishia kwamba familia ya Rais Tshisekedi haihusike katika uchimbaji madini Kivu kusini.

Niliona baadhi ya watu wenye nia mbaya wakimchafua mke wa raisi katika hili. Huo ni uongo! Mama yetu hahusiki kwa mbali wala kwa karibu katika uchimbaji wa madini”.

Pia, asasi hizo zimetangaza maandamano ya siku tatu mfululizo kwenye mpaka wa Congo na Rwanda kuanzia hii alhamisi, ili kupinga kile zinachokiita kuwa uvamizi wa Rwanda katika maeneo ya mashariki ya Congo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment