Bastola ya kiongozi wa Burkina Faso yazusha wasiwasi Ghana

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

fc
Maelezo ya picha,Bastola ilionekana wazi wakati Kapteni Ibrahim Traore (kushoto) akimsalimia Rais mpya wa Ghana John Mahama (kulia)

Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amezusha wasiwasi alipohudhuria hafla ya Jumanne ya kuapishwa kwa Rais wa Ghana, John Mahama akiwa na bastola kiunoni.

Baadhi wameelezea hatua hiyo isiyo ya kawaida, kuwa ukiukaji wa itifaki za kiusalama.

Wengine wameona ni ukosefu wa imani kwa uwezo wa maafisa wa Ghana kumlinda mkuu huyo wa serikali ya kijeshi ya Burkinabe.

Haijabainika iwapo Traore alikuwa na kibali cha kubeba silaha hiyo na serikali mpya ya Ghana haijajibu ombi la BBC la kutoa kauli yake.

Mahama aliapishwa baada ya kumbwaga kwa kura nyingi mgombea wa chama tawala, Mahamudu Bawumia katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Traore, alikuwa mmoja wa wakuu wa nchi 21 waliokuwepo, na ziara yake imekuja wakati kukiwa na mvutano wa kidiplomasia huko Afrika Magharibi.

Burkina Faso, pamoja na nchi nyingine mbili zinazoongozwa kijeshi – Mali na Niger, zimejitenga na umoja wa kikanda wa Ecowas na kuunda muungano wao wenyewe.

Mchambuzi wa masuala ya usalama Vladmir Antwi Danso amesema si kawaida kwa mkuu wa nchi kubeba silaha kwenye sherehe ya kuapishwa kwani usalama wa kiongozi anayezuru ni jukumu la mwenyeji.

Uhusiano kati ya Ghana na Burkina Faso umekuwa mbaya, haswa baada ya Rais wa zamani wa Ghana Nana Akufo-Addo kumshutumu Traore kwa kuwahifadhi mamluki wa Urusi.

Kuhudhuria kwa Traore katika hafla hiyo kumeonekana kuwa ishara muhimu ya kidiplomasia inayolenga kurekebisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment