Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais mteule wa Ghana, John Mahama, anatarajiwa kuapishwa leo baada ya kushindi uchaguzi wa mwezi uliopita.
Kwa mara ya kwanza, nchi hiyo pia itakuwa na Makamu wa Rais mwanamke, Profesa Jane Naana Opoku Agyemang.
Mahama amewahi kuhudumu kama Rais wa Ghana kuanzia 2012 hadi 2017.
Viongozi 21 wa nchi wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo katika ukumbi wa Black Star Square mjini Accra.
Anachukua hatamu ya uongozi wakati Ghana inajikwamua kutokana na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi.
Ghana kwa sasa inakabiliwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira, na iko chini ya mpango wa uokoaji wa IMF wa dola bilioni 3.
Mahama ameahidi kupunguza ushuru na kusaidia wajasiriamali ili kupunguza hali ngumu ya kiuchumi. Hata hivyo, Rais anayeondoka Nana Akufo Addo anadai uchumi umeimarika, kauli iliyopingwa na wabunge wa upinzani.
Raia wengi wa Ghana wana matumaini kwamba uzoefu wa Mahama kama rais wa zamani utamsaidia kutatua changamoto za kiuchumi za nchi hiyo.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.