Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),Constant Mutamba amezungumzia Januari 6, 2025 huko Kinshasa kuhusu hali ya wanachama wa magenge ya mijini waliokamatwa na kuhukumiwa kifo kama sehemu ya “Zéro Kuluna – Ndobo”, operesheni iliyofanywa kwa pamoja miaka ya hivi karibuni na wizara yake (mahakama) na ile ya Mambo ya Ndani.

Waziri wa Sheria amekariri kwamba, ikiwa DRC itadhamiria kutekeleza hukumu iliyotolewa, ni baada ya kuchoshwa na rufaa mbalimbalina wito ndipo hukumu ya kifo inatekelezwa.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mamlaka inasema imedhamiria kuekeleza adhabu ya kifo ili kukatisha tamaa ya ujambazi wa mijini ambao umekithiri hasa katika mji mkuu, ambako polisi wanafanya msako dhidi ya wahalifu, wahusika wa wizi, mauaji na aina nyingine za ukatili. Kesi zilisikilizwa ambapo makumi ya vijana walihukumiwa kifo.
Hakuna hukumu ya kifo iliyotekelezwa
Mnamo Januari 6, 2025, wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Kinshasa, mamlaka ilipuuza ukosoaji na wito mwingine kutoka kwa mashirika ya kimataifa na ya kitaifa yaliyopinga utekelezaji wa hukumu ya kifo.
Kesi kumi na moja zlisikilizwa tangu mwezi Desemba, amesema Waziri wa Sheria, Constant Mutamba. Vijana zaidi ya mia moja wa magenge yanayoitwa “Kulunas” walihukumiwa kifo mara ya kwanza.
Mia moja na ishirini na saba walihamishwa kutoka Kinshasa hadi gereza lenye ulinzi mkali kaskazini-magharibi, huko Angenga, na wengine sitini walipelekwa Luzumu, nje ya Kinshasa. Lakini hakuna hukumu ya kifo iliyotekelezwa.
“Mwendesha mashtaka wa umma lazima awasilishe ombi la msamaha wa rais”
Kwa sababu utaratibu ni mrefu na wahukumiwa wanapaswa kumaliza rufaa zao kabla ya hukumu inayowezekana. Constant Mutamba anasisitiza: “Ni wakati huu tu unapokwisha ndipo hukumu ya kifo inatekelezwa. Ingawa waziri huyo anasema kwamba mwendesha mashtaka wa umma, ambaye ameitwa kutekeleza hukumu ya kifo, lazima awasilishe ombi la msamaha wa rais. Mwisho wa siku, ni hakimu mkuu [rais wa nchi] ambaye anakuambia: “Ninakataa” au “Ninakubali adhabu ya kifo”. Hivi ndivyo sheria zetu zinavyosema. “
Ikiwa wafungwa walihamishwa, ni kwa sababu za kiusalama, anaongeza Waziri wa Sheria. Wafungwa hao ni hatari na wengi wao walirelea makosa yao: “Wengi wa wafungwa hawa, mbele yangu, walivunja pingu zao. Hii ni mbaya sana! Wamezoea kukabiliana na mahakama na vikosi vya usalama. “
Kuhamishwa kwao, hakusitishi haki yao ya kukata rufaa kwa mahakama za mamlaka zinazohusika, anasema waziri wa sheria.
Operesheni hii ya polisi iliyoambatana na kesi za waziwazi, iliyorushwa kwenye televisheni ya serikali, ilifanya iwezekane, kulingana na mamlaka, “kupunguza kwa kiasi kikubwa” uhalifu huko Kinshasa. Na kama uthibitisho, Waziri wa Sheria wa Kongo ameridhika, “kwa mara ya kwanza, watu wa Kinshasa walitumia sikukuu za mwisho wa mwaka na Mwaka Mpya bila kuwa na wasiwasi” na magenge.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.