Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Baada ya kuwezesha makubaliano kuhusu kudorora kwa uhusiano kati ya Somalia na Ethiopia katikati ya mwezi Desemba, Ankara sasa inajipanga kusaidia Sudani kutatua tofauti zake na Falme za Kiarabu. Mwishoni mwa wiki hii, mkuu wa jeshi la Sudani, ambaye anashutumu Abu Dhabi kwa kuwapa silaha wanajeshi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (FSR), amesema anaunga mkono upatanishi ambao Uturuki inapendekeza.
“Mpango” wa Ankara unaweza “kupelekea kupatikana kwa amani nchini Sudani” ambayo “inahitaji ndugu na marafiki kama Uturuki“, alitangaza mwishoni mwa wiki hii mkuu wa diplomasia ya Sudani, Ali Youssef, baada ya mkutano kati ya Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, mkuu wa jeshi la Sudani, na naibu waziri wa mambo ya nje wa Uturuki katika mji wa Port Sudan.
Mwishoni mwa mkutano huu, naibu waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alikuwa na jukumu la “kupeleka kwa Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, mapokezi mazuri ya viongozi wa Sudani kwa mpango [wake]” ulioanzishwa katikati ya mwezi wa Desemba kujaribu “kutuliza mizozo kati ya Sudani na Falme za Kiarabu”, ikishutumiwa kusambaza silaha kwa wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) – na hivyo kurefusha vita na mateso kwa raia wa Sudani.
“Moja ya shida ni kujua iwapo Uturuki itaweza kutoa chochote isipokuwa njia ya majadiliano”
Baada ya mkutano wake na Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki alisema kuwa “juhudi za pamoja” zitakuwa muhimu kufikia amani nchini Sudani. Katika suala hili, diplomasia ya Uturuki, iliyoanzishwa vyema katika Pembe ya Afrika, imesema iko tayari kuhamasisha “wahusika wengine wa kikanda kusaidia […] kukomesha mzozo huu”.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.