Syria: Mapigano makali kati ya makundi yanayounga mkono Uturuki na Wakurdi kaskazini mwa nchi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Zaidi ya wapiganaji 100 wameuawa katika siku mbili zilizopita katika mapigano kaskazini mwa Syria kati ya makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na Uturuki na vikosi vya Wakurdi wa Syria, Shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Syria (SOHR) limesema siku ya Jumapili Januari 5, 2025.

Kundi linalounga mkono Uturuki katika eneo la Manbij mwaka wa 2019.
Kundi linalounga mkono Uturuki katika eneo la Manbij mwaka wa 2019. AP

Tangu Ijumaa jioni, mapigano katika vijiji karibu na mji wa Manbij yamesababisha vifo vya watu 101, wanachama 85 wa makundi ya Wasyria yanayounga mkono Uturuki na 16 wa Syrian Democratic Forces (SDF, inayoongozwa na Wakurdi), mkurugenzi wa SOHR, Rami Abdel Rahmane, ameliambia hirika la habari la AFP.

Katika taarifa, SDF imedai kuzima “mashambulio yote ya mamluki wa Uturuki wanaosadiwa na ndege zisizo na rubani na ndege za Uturuki”. Makundi yanayoiunga mkono Uturuki yalianza tena mashambulizi yao dhidi ya FDS, wakati huo huo makundi ya waasi wa Kiislamu yalipoanzisha mashambulizi yao Novemba 27 dhidi ya majeshi ya Rais Bashar el-Assad, yaliyoondolewa madarakani siku kumi na moja baadaye. Walichukua miji ya Manbij na Tal Rifaat, kaskazini mwa mkoa wa Aleppo, kutoka kwa FDS na mapigano yameendelea tangu wakati huo, na kusababisha hasara kubwa ya kibinadamu.

Miji ya Kobane na Tabaqa yakabiliwa na tishio?

Kulingana na Rami Abdel Rahmane, lengo la wafuasi wa wanaounga mkono Uturuki ni kuchukua udhibiti wa miji ya Kobané na Tabaqa, kisha ile ya Raqqa na hatimaye kuwafukuza FDS kutoka maeneo wanayodhibiti. SDF inadhibiti maeneo makubwa ya kaskazini-mashariki na sehemu ya jimbo la Deir Ezzor (mashariki), ambapo Wakurdi waliweka utawala unaojitegemea baada ya kuondolewa kwa majeshi kutoka madarakani mwanzoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria mwaka 2011.

Uturuki; nchini jirani inaiona SDF kama nyongeza ya adui wake mkubwa, Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK, Wakurdi wa Kituruki). Na jeshi lake huwalenga mara kwa mara wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria na nchi jirani ya Iraq.

Kiongozi mpya wa Syria, mkuu wa kundi la waislamu wenye itikadi kali la Hayat Tahrir al-Sham (HTS), Ahmad al-Shareh, amesema SDF inapaswa kuingizwa katika jeshi la baadaye la Syria. Kundi la HTS liliongoza muungano wa makundi ya waasi ambao ulitangaza Desemba 8, baada ya kuingia Damascus, kuanguka kwa Assad ambaye alikimbilia Moscow. Muungano huu unadhibiti sehemu kubwa ya nchi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment