Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mkuu wa jeshi la Uganda Generali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mtoto wa Rais wa muda mrefu Yoweri Museveni, amesema anataka kumkata kichwa kiongozi mashuhuri wa upinzani nchini humo Bobi Wine.
Kainerugaba mara kwa mara hutoa machapisho yenye utata kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni pamoja na tishio la 2022 la kutaka kuivamia nchi jirani ya Kenya.
Katika chapisho kwenye X Jumapili jioni, Kainerugaba alisema babake aliyeitawala Uganda tangu 1986, ndiye mtu pekee anayemlinda kiongozi wa upinzani Bobi Wine dhidi yake.
“Kama Mzee hakuwepo, ningemkata kichwa leo,” ameandika Kainerugaba.
Bobi Wine, ambaye jina lake ni Robert Kyagulanyi, alimaliza wa pili nyuma ya Museveni katika uchaguzi wa urais wa 2021, alijibu kupitia X kwamba hapuuzi vitisho hivyo, na kusema kumekuwa na majaribio kadhaa ya kuuawa siku za nyuma.
Kainerugaba alijibu: “Hatimaye! Nimekuamsha? Kabla sijakukata kichwa, uturudishie pesa tulizokukopesha,” akidai kuwa hapo awali serikali ilikuwa imemnunua Wine ili kudhoofisha upinzani.
Wasemaji wa serikali na Kainerugaba mwenyewe hawakupatikana mara moja kutoa maoni yao. Huku msemaji wa jeshi akikataa kutoa maoni yake.
Wine, mwanamuziki maarufu aliyegeuka kuwa mwanasiasa ni mpinzani mwenye nguvu dhidi ya Museveni. Alikataa matokeo ya uchaguzi wa 2021, kwa madai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.