Kusini: Mazungumzo ya amani ya Tumaini yaanzishwa tena Nairobi, Kenya

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mazungumzo ya amani ya Tumaini kuhusu Sudan Kusini, yameanzihwa tena jijini Nairobi, Kenya siku ya Jumatatu Januari 6, 2024. Mazungumzo haya yanahusisha serikali ya mpito ya Sudani Kusini, upinzani na makundi yenye silaha ambao hawakutia saini makubaliano ya amani ya mwaka 2018. Mazunguzmo hayo yalimaliza miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Salva Kiir (picha yetu) anatoa wito wa kuwajibika kwa wapinzani wake, na anawaomba “ndugu zake waonyeshe uzalendo na kuweka maslahi ya nchi mbele”
Salva Kiir (picha yetu) anatoa wito wa kuwajibika kwa wapinzani wake, na anawaomba “ndugu zake waonyeshe uzalendo na kuweka maslahi ya nchi mbele”

Mazungumzo ya Tumaini tayari yamekatishwa mara kadhaa. Mnamo mwezi Desemba 2024, Rais wa Kenya William Ruto aliingilia kati kibinafsi na kuanzisha upya mchakato ambao bado unaonekana kuwa mgumu.

Kimsingi, wote wanakubaliana: mwafaka lazima upatikane katika mwaka wa 2025. Wakati wa akiwatakiwa Heri ya mwaka Mpya wananchi wake, Rais Salva Kiir alisema Uchaguzi Mkuu unapaswa kufanyika mwaka 2026. Hapo awali ulipagnwa kufanyika mwezi Desemba 2024, serikali iliamua kwa upande mmoja kuuahirisha.

“Uzalendo”

Salva Kiir anatoa wito wa kuwajibika kwa wapinzani wake, na anawaomba “ndugu zake waonyeshe uzalendo na kuweka maslahi ya nchi mbele”. Haya ni maoni ya Pagan Amum Okiech, rais wa True-SPLM, kundi lililojiongoa katika chama kilicho madarakani kwa sasa. Katika hotuba yake ya kuwatakia wananchi wake Heri ya Mwaka Mpya, anawaomba Wasudan wote “kuunga mkono mchakato wa Tumaini”. Lakini pia anailaumu serikali ya mpito kwa kubadili msimamo wake mara kwa mara, jambo ambalo, kulingana naye, linahatarisha majadiliano.

Uchaguzi huru na wa kidemokrasia

“Ili mazngumzo ya Tumaini yaweze kufanikiwa, kunahitajika mabadiliko ya kimataifa katika mtazamo wa kisiasa,” Edmund Yakani, mkurugenzi wa Shirika la Uwezeshaji Jamii kwa Maendeleo (CEPO), katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. Kwake, majadiliano yanapaswa kulenga somo moja pekee: kuandaa uchaguzi huru na wa kidemokrasia mwaka wa 2026.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment