Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kiongozi wa upinzani wa Msumbiji ambaye, amekuwa akiongoza maandamano ya wiki kadhaa kupinga uchaguzi wenye utata kutoka uhamishoni, anasema atarejea nchini siku ya Alhamisi.
Venancio Mondlane alisema (kwenye mitandao ya kijamii) atawasili kabla ya kuapishwa kwa rais mpya.
Daniel Chapo wa chama tawala cha Frelimo anatazamiwa kuapishwa wiki ijayo.
Uthabiti wa Msumbiji umeathiriwa vikali katika wiki chache zilizopita.
Ikiwa kiongozi wa upinzani Venacio Mondlane atarejea nchini – kama alivyoahidi – msukosuko zaidi unaweza kuendelea.
Ghasia za baada ya uchaguzi nchini Msumbiji zilichochewa na kile ambacho wengi, wakiwemo waangalizi wa uchaguzi, waliona kama kura ya maoni yenye dosari kubwa ambayo iliongeza miaka 49 ya chama cha Frelimo.
Kuapishwa kwa Daniel Chapo kunatarajiwa baada ya siku kumi.
Hakuna kitu cha kunachoashiria kupatikana kwa utulivu hivi karibuni nchini Msumbiji.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.