Aliyekuwa gavana wa Benki ya Mauritius akamatwa kwa madai ya ubadhirifu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Gavana huyo wa zamani wa Benki ya Mauritius alikamatwa Ijumaa Januari 3 kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ubadhirifu wa fedha za umma. Harvesh Seegolam alikuwa chini ya hati ya kukamatwa tangu katikati ya mwezi wa Desemba. Alijiuzulu muda mfupi baada ya uchaguzi wa wabunge mnamo mwezi wa Novemba 2024, kufuatia kuingia mamlakani kwa serikali mpya. Mamlaka mpya zinamshuku kuwa alihamisha kinyume cha sheria kiasi cha dola milioni moja kwenye akaunti ya benki nje ya nchi.

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Mauritius Port-Louis.
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa Mauritius Port-Louis. Thierry/Wikipédia

Gavana wa zamani wa Benki ya Mauritius alikamatwa Ijumaa Januari 3, 2025, katika uwanja wa ndege wa kisiwa hicho na kikosi cha fedha. Harvesh Seegolam anashukiwa kupanga uhamishaji haramu wa dola milioni moja kwa kampuni yenye uhusiano wa kisiasa unaotiliwa shaka. Kesi hiyo ilizuka mnamo Novemba 2024, baada ya kujiuzulu siku moja baada ya uchaguzi wa wabunge wa Novemba 10, 2024. Benki kuu iliwasilisha malalamiko ya udanganyifu, ikitaja kuwepo kwa uhamisho unaotiliwashaka uliofanyika katikati ya kampeni za uchaguzi. .

“Ubadhirifu”

Uongozi mpya wa Benki ya Mauritius umeamua: “Kwa hakika kulikuwa na ubadhirifu” na uhamisho huu. Hata hivyo, gavana huyo wa zamani alikuwa tayari ameondoka nchini wakati malalamiko yalipowasilishwa. Hii ilisababisha polisi kutoa hati ya kukamatwa mnamo Desemba 16. Siku ya Ijumaa asubuhi, alikamatwa aliposhuka kwenye ndege.

Njama?

Baada ya usiku kucha akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kuhojiwa kwa muda mrefu, Harvesh Seegolam aliachiliwa Jumamosi Januari 4, 2025, kwa shtaka la muda la “kula njama ya kulaghai”. Wachunguzi sasa wanavutiwa kwa karibu na uwezekano wa kuhusika kwa ndani katika Benki ya Mauritius na wanachunguza uhusiano ambao unaweza kuwepo na baadhi ya viongozi wa kisiasa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment