Burma: Utawala wa kijeshi wasamehe maelfu ya wafungwa kwa ajili ya maadhimisho ya uhuru

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Utawala wa kijeshi wa Burma umetangaza siku ya Jumamosi, Januari 4, msamaha wa maelfu ya wafungwa, hatua ya kila mwaka kwa mnasaba wa maadhimisho ya uhuru wa nchi hiyo.

FILE - Senior Gen. Min Aung Hlaing, head of the military council, inspects officers during a parade to commemorate Myanmar's 78th Armed Forces Day in Naypyitaw, Myanmar, on March 27, 2023. (AP Photo/A
Jenerali Min Aung Hlaing, Mkuu wa baraza la kijeshi, akiwakagua maafisa wakati wa gwaride la kuadhimisha Siku ya 78 ya Wanajeshi wa Myanmar huko Naypyitaw, Myanmar, Machi 27, 2023. AP – Aung Shine Oo

Zaidi ya wafungwa 5,800, ikiwa ni pamoja na baadhi ya wageni 180, hivi karibuni watanufaika na hatua hii, utawala wa kijeshi umebainisha katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP, wakati Burma inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 77 ya uhuru wake, Januari 4, 1948, kutoka kwa Uingereza.

Hakuna habari iliyofichuliwa kuhusu sababu za kufungwa kwao au uraia wa raia wa kigeni wanaohusika ambao watafukuzwa baada ya kuachiliwa, shirika la habari la Ufaransa linabainisha zaidi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment