Senegal: Upi mustakabali wa APR na kiongozi wake Macky Sall?

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Baada ya kumaliza muda wake kama rais wa Senegal mwezi Aprili, alichaguliwa kuwa mbunge mwezi Novemba na kujiuzulu mamlaka yake katika Bunge, mkuu huyo wa zamani wa nchi sasa anataka kustaafu katika chama chake alichoanzisha  mwaka 2008. Uamuzi ambao, hata hivyo, haimzuii Macky Sall, sawa na Muungano wa Jamhuri (APR) anaoongoza, kufikiria mustakabali wa chama hicho.

Macky Sall, aliyekuwa rais wa Senegal wakati huo, mjini Brussels, Oktoba 25, 2023.
Macky Sall, aliyekuwa rais wa Senegal wakati huo, mjini Brussels, Oktoba 25, 2023. REUTERS – JOHANNA GERON

Rais wa zamani wa Senegal Macky Sall amebainisha hili kwa vyombo vya habari vya mtandaoni Siri Dakar: ana nia ya kujiondoa katika majukumu yake ya kisiasa ndani ya Alliance for the Republic (APR), chama alichoanzisha mwaka 2008. Walipohojiwa na wanahabari, wasaidizi wake wanaeleza kwamba rais wa zamani anataka “kujiweka kando kidogo”.

Kwa mtazamo huu, Macky Sall kwa hivyo anapaswa kupewa urais wa heshima wa APR ili kudumisha uhusiano na chama, bila kulazimika kusimamia shughuli zake za kila siku, anabainisha mmoja wa marafiki zake wa karibu. Maendeleo haya yangeiwezesha, miongoni mwa mambo mengine, kutoa muda wa shughuli zake za kimataifa.

“Mwisho wa mzunguko”

Mkutano wa makada wa chama ulifanyika wiki iliyopita ili kuzingatia hali ya baadaye ya utawala wa chama, mmoja wa washiriki wake ameambia RFI. Lakini hakujazungumzwa juu ya suala la “kumrithi” rais wa zamani wa nchi kwenye nafasi ya katika chama, kinabainisha zaidi chanzo hiki, ambacho hata hivyo kinatambua kwamba baada ya miaka 12 madarakani, ni “mwisho wa ‘mzunguko’ na kwamba ni ‘ muhimu kufikiria juu ya malengo mapya.

Licha ya kushindwa vibaya katika uchaguzi wa wabunge Novemba mwaka jana, APR inakusudia kuchukua nafasi ya mpinzani wa kwanza dhidi ya mamlaka mpya. Mabadiliko haya yote yaliyoanzishwa wakati wa kongamano lisilo kuwa la kawaida mnamo mwezi Desemba 2023 yataidhinishwa haraka. Ingawa hakuna tarehe kamili iliyowasilishwa kwa hatua hii, kongamano la chama lifanyika katika miezi ijayo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment