Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Katika kesi ya kiongozi wa chama cha MoDeL kwa “matusi na kashfa” dhidi ya mkuu wa utawala wa kijeshi, Jenerali Mamadi Doumbouya, mwendesha mashtaka ameomba kifungo cha miaka miwili jela dhidi ya mshtakiwa, siku ya Alhamisi Januari 2. Mawakili watano wa Aliou Bah wamezungumza kwa zaidi ya saa nne mbele ya mahakama ya mwanzo ya Kaloum, mjini Conakry, kumtetea mteja wao, huku wakikana mashtaka na kuomba aachiliwe huru.

Wasiwasi ulionekana kwenye nyuso za kila mtu, siku ya Alhamisi, Januari 2, wakati ilipokuwa ikisikilizwa kesi ya mwanasiasa wa upinzani Aliou Bah kwa “matusi na kashfa” dhidi ya mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Guinea, Jenerali Mamadi Doumbouya, mbele ya mahakama ya mwanzo ya Kaloum, huko Conakry.
Afisa wa mawasiliano kwa wanawake kutoka chama cha MoDeL, chama cha Aliou Bah, Kadiatou Barry anahoji, hasa, kuhusu mwelekeo ambao Guinea inachukua: “Tunaishi katika nchi ambayo hatuthubutu tena kusema chochote, ambapo kila mtu ana haki ya kusema kila kitu, isipokuwa kuzungumzia serikali na kasoro za Serikali. Kwa hivyo tuko kwenye udikteta! Tutaendelea hivi mpaka lini? »anasema.
Kwa upande wake, Wakili Houlématou Bah, mwanasheria wa upande wa utetezi, amewashambulia majaji ambao anawashutumu kwa “kutafuta faida” ili kuwatia hatiani watu wasio na hatia. “Ninachukizwa kuona kwamba hata katika karne ya 21, kuna majaji wanaotumikia Serikali, ili tu kwa ajili ya maslahi yao, au kunufaika na uteuzi wao. Matakwa ya mwendesha mashtaka wa umma ni matakwa ambayo yanaaibisha utawala wa sheria, “anasema.
“Tamko la vita juu ya uhuru wa kujieleza”
Mwishoni mwa ombi la mwendesha mashtaka Mohamed Bangoura, Wakili Antoine Pépé Lamah, ambaye pia anamtetea Aliou Bah, ameionya mahakama iwapo itashawishiwa kumfuata mwendesha mashtaka wa umma. “Kwangu mimi, ombi hili ni tangazo la vita dhidi ya uhuru wa kujieleza. Ikiwa mahakama itawafuata, basi itakuwa imesaini kifo chake kwa njia ya kisheria,” anaeleza.
Aliou Bah ambaye alikamatwa Desemba 26 mwaka jana kwenye mpaka kati ya Guinea na Sierra Leone alipokuwa akielekea Freetown, anazuiliwa tangu Jumatatu Desemba 30 katika gereza la kiraia la Conakry.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.