Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Viwango vipya vya uzalishaji wa gesi chafu, CO2, vilianza kutumika katika EU mnamo Januari 1, 2025. Shinikizo la ziada linawekwa kwa makampuni ya kutengeneza magari ya Ulaya, pamoja na hatari ya kutozwa faini. Suluhisho moja tu kwao: kuongeza mauzo ya magari ya umeme. Changamoto ya kweli katika soko ambayo imekuwa ikipungua kwa miezi kadhaa

Ingawa EU imepunguza kiwango chake cha uzalishaji wa hewa chafu ya CO2 mnamo Januari 1, angalau theluthi moja ya mauzo ya makampuni mengi ya magari sasa italazimika kuwa mauzo ya magari ya umeme ili kuepusha faini kubwa. Iwapo makampuni ya kutengeneza magari ya Ulaya yatashindwa kufikia malengo yaliyowekwa kwa mwaka wa 2025, yanaweza kukabiliwa na faini inayokadiriwa kufikia euro bilioni 15 kwa jumla.
Lakini katika kipindi cha miezi kumi na moja ya kwanza ya mwaka 2024, mauzo ya magari ya umeme yaliwakilisha tu zaidi ya 13% ya jumla ya mauzo huko Ulaya. Hii inasumbua wazalishaji. Ili wao kuepuka faini zinazotolewa na kanuni mpya za Ulaya, gari moja kati ya matano yanayouzwa itabidi liwe la umeme.
Hatari ya kupoteza uwezo wa uwekezaji
ACEA, inayowakilisha sekta hiyo barani Ulaya, inaomba Brussels kutotumia adhabu hizi nzito. Inabaini kwamba hii inaweza kusababisha hasara ya karibu euro bilioni 16 katika uwezo wa uwekezaji kwa wmakampuni ya kutengeneza magari. Kutokana na kupanda kwa umeme na uboreshaji wa injini za mafuta, makampuni ya kutengeneza magari hadi sasa yameheshimu kiwango kinachojulikana kama Uchumi wa Wastani wa Mafuta wa (CAFE) “Corporate Wastani wa Uchumi wa Mafuta”, ambayo yanakabiliana nayo, chini ya adhabu ya faini kubwa, kuheshimu wastani wa kila mwaka wa uzalishaji kwa kila gari inayouzwa.
Kulingana na takwimu za hivi karibuni kutoka ACEA, na karibu vitengo 125,000 vilivyouzwa, magari ya umeme yalipungua mwezi Oktoba katika masoko kuu (Ujerumani, Ufaransa, Italia) lakini yalibakia imara katika nchi ambazo tayari zimetumia umeme (Uholanzi, Denmark, Ubelgiji). Huko Ufaransa, kupunguzwa kwa bonasi ya ikolojia, iliyopitishwa dakika za mwisho na serikali ya Barnier na kuanza kutumika mnamo Januari 1, haitasaidia kufufua mauzo.
Mbali na magari ya umeme, mauzo ya magari ya mafuta pia yako nusu mlingoti. Jambo ambalo pia linazua swali la kukithiri kwa uzalishaji wa viwanda. Volkswagen inapanga kupunguza kazi 35,000 nchini Ujerumani ifikapo mwaka 2030, au 30% ya wafanyakazi wake, na viwanda vya Stellantis vinafanya kazi kwa thuluthi mbili ya uwezo wao.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.