UNAPOKUA NA MATARAJIO MAKUBWA KUTOKA KWA MARAFIKI .

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moja ya “dissappointment” kubwa unaweza kuipata kwenye maisha yako, ni pale unapokuwa na MATARAJIO MAKUBWA sana kutoka kwa marafiki zako na ikawa tofauti.

Kitu kimojawapo nimejifunza ni kuwa marafiki WOTE HAWAKO SAWA.

Usipoweza kuwatofautisha, hautajua UWAWEKE WAPI na wakusaidie kwenye LIPI.

“Convinience Friends” – Hawa ni marafiki kwa sababu mko ofisi moja mnasaidiana, mnaabudu pamoja n.k

“Seasonal Friends” – Hawa mnaungwanishwa na majira fulani ya maisha. Mnaweza kukutana kwenye interview, mko safarini wote, vikao vya harusi n.k

“Destiny Friends” – Hawa mnaunganishwa na kusudi la maisha. Mungu amewaandaa ili watembee na wewe kukuvusha kuelekea hatima yako. Hawa huwa wanajitoa kwa kiwango KIKUBWA sana (Muda, Mali, Nguvu n.k).

Kila kundi tunawahitaji, ila ukikosa hawa wa kundi la mwisho ni ngumu kupiga hatua kwenye maisha.

Mwaka huu jitahidi KUWATAMBUA na KUWATUNZA, wako wachache sa na hapa duniani.

Kama umeipenda makala hii…

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment