Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nigeria inajibu baada ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Australia kutoa onyo ikiwashauri vikali raia wake kutosafiri katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika kutokana na hatari kubwa ya utekaji nyara na ugaidi.

Kwenye tovuti ya Smartraveller ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Australia, onyo liko wazi: inapendekezwa sana kutosafiri kwenda Nigeria – “pamoja na mji mkuu Abuja”, “kutokana na hali tete ya usalama, vitisho vya ugaidi, utekaji nyara, uhalifu wa kivita na machafuko ya kijamii.”
Wasafiri wanahimizwa kuepuka kabisa majimbo 24 kati ya 36 ya Nigeria: maeneo yote ya kaskazini-mashariki, kaskazini-magharibi na kusini mashariki mwa Nigeria yamejumuishwa katika orodha hii, ambayo pia inajumuishamji mkuu wa shirikisho, jimbo la Abuja.
Mapendekezo haya, yaliyosasishwa mnamo Desemba 20, kwa wazi hayakuifurahisha Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria, ambayo haikuchelewa kutoa ushauri wake kwa raia wake wanaotaka kusafiri kwenda Australia.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyorushwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Wizara inaomba raia wa Nigeria wanaowasili nchini Australia “kuwa waangalifu dhidi ya ongezeko la matukio ya kibaguzi na yanayopinga Waislamu […] yanayohusiana na muktadha wa kimataifa na yanayoongeza hatari ya machafuko nchini Australia. Mamlaka ya Nigeria pia inanyooshea kidole “kesi za ubaguzi, unyanyasaji au matusi dhidi ya wageni” katika baadhi ya miji ya Australia.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.