Italia yamuita balozi wa Iran huku ikitaka mwanahabari aachiliwe

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

fv
Maelezo ya picha,Cecilia Sala

Wizara ya mambo ya nje ya Italia imemwita balozi wa Iran siku ya Alhamisi na kutaka aachiliwe mwanahabari Cecilia Sala mara moja, ambaye amezuiliwa Tehran tangu Desemba 19, alipokuwa akifanya kazi chini ya viza ya uandishi wa habari.

Wizara hiyo imesema katika taarifa yake kuwa ina “wasiwasi mkubwa” juu ya kuzuiliwa kwa Sala na kusisitiza haja ya kutendewa haki na kuheshimiwa kwa haki zake za kibinadamu.

Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Italia, Riccardo Guariglia, amesema wafanyakazi wa ubalozi wa Tehran wanapaswa kuruhusiwa kumtembelea Sala na kumpa “vifaa ambavyo amenyimwa,” wizara hiyo imesema.

Shirika rasmi la habari la IRNA la Iran liliripoti Jumatatu kwamba Sala amekamatwa kwa “kukiuka sheria za Jamhuri ya Kiislamu.” Lakini halikutoa taarifa zaidi.

Sala alizuiliwa siku tatu baada ya mfanyabiashara wa Iran, Mohammad Abedini, kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Malpensa wa Milan, Italia kwa waranti ya Marekani, kwa madai ya kusambaza vifaa vya ndege zisizo na rubani ambazo Washington inasema zilitumika katika shambulio la 2023 lililoua wanajeshi watatu wa Marekani huko Jordan.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment