DR Congo: Tshisekedi atangaza msamaha wa rais kwa wafungwa.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa DRC Félix Tshisekedi, ametangaza msamaha kwa wafungwa mbalimbali, lakini haijafahamika iwapo wafungwa wa kisiasa wa kutoka vyama vya upinzani kama Jean-Marc Kabund, Jacky Ndala na  Seth Kikuni wapo kwenye orodha hiyo.

Jean-Marc Kabund akiondoka katika Mahakama, Septemba 5, 2022.
Jean-Marc Kabund akiondoka katika Mahakama, Septemba 5, 2022. © RFI / Pascal Mulegwa

Orodha ya wafungwa hao waliopata msamaha huo wa rais Tshisekedi haijfahamika, lakini ripoti za ndani zinasema tume maalum iliyoundwa kutekeleza hatua hiyo, inatathmini ni wafungwa gani wanapaswa kuachiwa huru.

Waziri wa masuala ya Haki, Constant Mutamba, ameahidi kuwa mchakato huo utakuwa wazi na utakamilika baada ya mwezi mmoja.

Wanaotarajiwa kuachiwa huru ni wale ambao wamehukumiwa jela chini ya miaka metano, ambapo na kuachiwa huru, huenda wafungwa wengine wakapunguziwa kifungo.

Moïse Katumbi mwanasiasa wa upinzani nchini DRC ( Mwenye kofia) akiwa na mwenzake  Seth Kikuni
Moïse Katumbi mwanasiasa wa upinzani nchini DRC ( Mwenye kofia) akiwa na mwenzake Seth Kikuni © Alexis Huguet / AFP

Wale waliohukuliwa adhabu ya kifo, kifungo hicho kitapunguzwa kuwa hadi maisha jela, na wale waliofungwa maisha, kifungo chao kitapunguzwa hadi miaka 20 jela.

Hata hivyo, wale waliofungwa kwa sababu ya ubakaji, wizi wa fedha za uma na kutishia usalama wa taifa hawatanufaika na msamaha huo wa rais Tshisekedi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment