Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Ufaransa inalaani mashambulizi ya Israel kwenye hospitali za Gaza kufuatia shambulizi dhidi ya Kamal Adwan kaskazini mwa eneo hilo mwishoni mwa juma lililopita. Zaidi ya watu 240 walikamatwa, akiwemo mkurugenzi wa taasisi hiyo, akishutumiwa na Israel kuwa mwanaharakati wa Hamas. Madhara ya shambulio: Hospitali ya Kamal Adwan haitumiki. Jambo ambalo linafanya upatikanaji wa huduma za afya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kuwa mgumu zaidi.
“Mfumo wa afya umeharibiwa. ” Hivi ndivyo Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu inavyoelezea hali katika eneo hili ambalo Wagaza 75,000 bado wanaishi. Kati ya hospitali tatu kubwa, hakuna chochote kilichosalia. ICRC pia imetoa wito wa kuheshimiwa na kulindwa vituo vya matibabu kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu.
“Ulinzi huu ni wajibu wa kisheria na umuhimu wa kimaadili kuhifadhi maisha ya binadamu,” taarifa hiyo kwa vyombo vya habari imeongeza, ikibainisha kuwa hospitali ni muhimu kusaidia watu wagonjwa au waliojeruhiwa wakati wa vita.
WHO inaitaka Israel kumwachilia huru mkurugenzi wa hospitali Kamal Adwan
“Hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Ukanda wa Gaza imekuwa haifanyi kazi tangu shambulio la Israeli, kuhamishwa kwa lazima kwa wagonjwa na wafanyakazi na kuzuiliwa kwa mkurugenzi wake. Hatujui alipo. Tunataka aachiliwe mara moja,” Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameandika kwenye ukurasa wake wa X.
“Hospitali za Gaza kwa mara nyingine tena zimekuwa uwanja wa vita na mfumo wa afya unatishiwa pakubwa,” amesema.
Siku ya Jumamosi, jeshi la Israel lilibaini kufuatia shambulio lake lililozinduliwa siku ya Ijumaa, kwamba limemkamata mkurugenzi wa hospitali ya Kamal Adwan, Dk Hossam Abou Safiya.
Baada ya jeshi la Israel kuvamia, wagonjwa 15 na wahudumu 70 kutoka Hospitali ya Kamal Adwan walikimbilia katika hospitali ya Indonesia. Lakini hali huko ni ya kutisha vile vile: “Si chochote zaidi ya jengo lenye wahudumu wa afya wachache na vifaa vichache,” amesema msemaji wa Shirika la Afya Dunianii, ambaye timu yake iliweza kwenda huko Jumapili. Wagonjwa mahututi zaidi pia walihamishiwa hospitali moja katikati mwa Gaza.
85% ya miundo ya matibabu “imeharibiwa”
Hatimaye, hospitali ya al-Awda huko Jabalia, inayopatikana kaskazini, iko chini ya mkazo mkubwa, kwa sababu ni ya mwisho katika sekta hii kufanya kazi.
Katika Ukanda wa Gaza, 85% ya miundo ya matibabu “imeharibiwa” kulingana na Shirika la Madaktari wa Dunia. Shirika hili linashutumu “mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya miundo ya afya na wafanyakazi katika ukiukaji kamili wa sheria za kimataifa na za kibinadamu. “
Baridi imeingia Ukanda wa Gaza. Kwa sasa ni 10°C na mvua ni nyingi. Hali ya maisha ambayo tayari ni hatari inazidi kuwa mbaya na ina athari ya moja kwa moja kwa afya ya wakaazi wa Gaza. Wakati huo, wahudumu wa afya wamegundua kuwa maambukizo ya kupumua yanaongezeka.
“Hali ya maisha tayari ni mbaya, katika makazi ya muda. Tunapaswa kufikiria mahema ambayo, siku hizi, yamesombwa na mvua, na baridi, na chakula kidogo sana kikiingia katika Ukanda wa Gaza,” anasema Caroline Bedos, mkuu wa kitengo cha Mashariki ya Kati katika shirika la Madakarti wa Dunia “Médecins du monde”. “Kuna mablanketi machache, hakuna joto kwa wazi. Kuna mahema ambayo yamefurika maji na yana unyevu kupita kiasi na hivyo kusababisha maambukizo na kuenea kwa magonjwa. “
Anaendelea: “Kwa hiyo, tunachokiona ni ongezeko la huduma ya matibabu kwa magonjwa ya kupumua na kuzorota kwa afya ya watu. Pia tuliweza kuona vifo kutokana na baridi, hivi ndivyo mamlaka ya Gaza inavyoripoti, ambayo inataja vifo saba wakiwemo watoto sita,” anabainisha Caroline Bedos.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.