Kenya: Polisi wakandamiza maandamano ya amani dhidi ya utekaji nyara wa wapinzani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Makumi ya waandamanaji wa Kenya waliitikia Jumatatu Desemba 30, 2024 wito wa kupinga wimbi jipya la utekaji nyara wa wapinzani. Takriban waandamanaji hamsini wa amani, akiwemo Seneta Okiya Omtatah, walikamatwa Nairobi, Mombasa na Eldoret. Na takriban watu wanne waliteswa katika kituo kikuu cha polisi cha Nairobi.

Mwandamanaji aliyekamatwa na polisi wakati wa maandamano ya kupinga kutekwa nyara kwa wapinzani mnamo Desemba 30, 2024 huko Nairobi, Kenya.
Mwandamanaji aliyekamatwa na polisi wakati wa maandamano ya kupinga kutekwa nyara kwa wapinzani mnamo Desemba 30, 2024 huko Nairobi, Kenya. © Andrew Kasuku / AP

Maandamano hayo hata hivyo yalikuwa ya amani: umati uliashiria ishara za baadhi ya waliopotea, wakitaka waachiliwe na kukomesha utekaji nyara. Polisi walipoanza kurusha mabomu ya machozi, waandamanaji hao walikataa kuondoka na kuimba wimbo wa taifa.

Wimbi jipya la utekaji nyara, katika chimbuko la maandamano hayo, linawahusu hasa vijana waliomkosoa Rais William Ruto kwenye mtandao. Wawili kati yao walichapisha picha iliyotengenezwa kwa kutumia akili ya bandia ikimuonyesha mkuu wa nchi akiwa amelala kwenye jeneza.

Vikosi vya usalama vya Kenya vinashutumiwa kuwa nyuma ya dazeni za visa vya utekaji nyara tangu maandamano ya kuipinga serikali ya mwezi Juni na Julai 2024. Zaidi ya nusu ya watu waliotoweka wakati huo bado hawajapatikana hadi leo. Tangu mwanzoni mwa mezi Desemba, watu sita wapya waliotoweka wameripotiwa.

Polisi ya Kenya imekana kuhusika na kutoweka kwa watu hao. Siku ya Ijumaa Desemba 27, 2024, baada ya kukosolewa na watetezi wa haki za binadamu na viongozi kadhaa wa kisiasa, Rais William Ruto aliahidi “kukomesha utekaji nyara”.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment