Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wakati wa hotuba kwa taifa iliyotolewa mbele ya mabunge yote mawili, rais wa Algeria, aliyechaguliwa tena kwa muhula wa pili mwanzoni mwa mwezi Septemba, ameshambulia vikali Ufaransa mnamo Desemba 29, 2024. Abdelmadjid Tebboune pia amezungumza kwa mara ya kwanza kukamatwa kwa Boualem Sansal, mwaandishi, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria katikati mwa mwezi Novemba huko Algiers. Maelezo.

Rais Abdelmadjid Tebboune alihutubia raia wa Algeria siku ya Jumapili na kuishambulia vikali Ufaransa. Alirejelea kwenye maswali ya kumbukumbu katika “hotuba kwa taifa” iliyotolewa mbele ya mabunge yote mawili. Kwa mujibu wa dondoo za hotuba yake iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya ofisi ya rais, kiongozi huyo wa Algeria anatoa wito kwa Paris kutambua uhalifu wake nchini Algeria. Ingawa uhusiano kati ya Paris na Algiers uko chini kabisa, anadai ishara fulani kutoka Ufaransa zinazohusiana na kipindi cha ukoloni (1830-1962).
“Wafaransa lazima wakubali kwamba waliwaua na kuwaangamiza Waalgeria,” amebainisha Rais Abdelmadjid Tebboune, akirejelea wakati wa ukoloni na vita vya uhuru wa Algeria.
Mkuu huyo wa nchi pia aliitaka Ufaransa kusafisha maeneo yaliyochafuliwa ya majaribio ya nyuklia kusini mwa nchi: “Umekuwa nguvu ya nyuklia na umetuacha na magonjwa. Njoo usafishe! ” Anabainisha kuwa nchi yake haidai fidia, “bali utu wa mababu zetu na raia wetu”, alieleza.
Kwa wale ambao, leo, huko Ufaransa, wanasifu faida za ukoloni, kiongozi wa Algeria anajibu kwamba “iliiacha Algeria kuwa magofu”: 90% ya Waalgeria hawakujua kusoma na kuandika wakati wa uhuru, aliongeza.
Akirejelea swali la Sahrawi, alithibitisha kwamba “wazo la uhuru ni wazo la Wafaransa na sio la Morocco“, akisisitiza kwamba chaguzi za makazi wanazopendekeza kwa swali la Sahara Magharibi ni “chaguo kati ya uovu na mbaya zaidi inapotokea suala la kuondoa ukoloni na kujitawala.
Kwa mara ya kwanza, Rais Abdelmadjid Tebboune pia alirejelea katika kukamatwa katikati yamwezi Novemba huko Algiers kwa mwandishi, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria Boualem Sansal.
Rais wa Algeria anaelezea mwandishi kama tapeli na baba asiyejulikana. Anasema Sansal anatumwa na Ufaransa kudai kuwa nusu ya Algeria ni ya taifa lingine la Morocco. Mwandishi huyo amekuwa kizuizini tangu mwezi Novemba kwa kuhatarisha usalama wa taifa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.