Ajali ya ndege Muan: Mamlaka yaomba ukaguzi wa ndege za Boeing, maombolezo ya kitaifa yatangazwa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini Korea Kusini, ajali ya ndege usiku wa Jumamosi Desemba 28 kuamkia Jumapili Desemba 29, 2024 ilisababisha vifo vya watu 179. Ndege hiyo ilijaribu kutua kwa mara ya kwanza na ilionekana kuwa na matatizo kadhaa ya vifaa vya kutua. Watu wawili tu walinusurika, wafanyakazi wawili, mwanamume na mwanamke. Korea Kusini inapanga kufanya ukaguzi wa ndege zake aina ya Boeing. Rais wa mpito ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa.

Korea Kusini, Desemba 30, 2024, Kaimu rais Choi Sang-mok amezuru eneo la ajali kwa ajili ya sherehe za ukumbusho.
Korea Kusini, Desemba 30, 2024, Kaimu rais Choi Sang-mok amezuru eneo la ajali kwa ajili ya sherehe za ukumbusho. AP – Ahn Young-joon

Kaimu rais ameagiza ukaguzi wa jumla wa shughuli zote za ndege nchini. “Kuhusu ukaguzi wa kina, ripoti za matengenezo ya mifumo muhimu kama vile injini na vifaa vya kutua vitachunguzwa kwa uangalifu kwa ndege 101 za kampuni sita zinazotumia aina sawa na ile iliyofanya ajali,” Naibu Waziri mwenye dhamana wa Anga, Joo Jong-wan amsema , akibainisha kuwa utaratibu huo utaendelea hadi Januari 3. Ni Boeing 737-800 ambazo zinalengwa haswa na tangazo hili.

Nchi hiyo imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku saba na bendera kupeperushwa nusu mlingoti. Katika eneo la ajali, utafutaji unaendelea kupata mabaki ya binadamu. Kupitia alama za vidole na vipimo vya DNA, mamlaka imeweza kutambua robo tatu ya waliofariki, linaripoti sirika la habari la AFP. Kaimu Rais Choi Sang-mok amezuru eneo la mkasa kwa ajili ya sherehe za ukumbusho.

Katika wilaya ya Yongsan, katikati mwa mji mkuu, Suyeon anarejea nyumbani. Mwanafunzi anapozungumza kuhusu ajali hiyo, machozi yanamtoka: “Nilikuwa nikifanya kazi nilipokutana na makala. Mwanzoni nilishangaa, sikufikiri ilikuwa mbaya kiasi hicho. Leo nimeumia sana. Inasikitisha sana. Natumai hii haitatokea tena. Inavunja moyo wangu. »

Jiha, 24, alifahamu kuhusu hilo adhuhuri Jumapili. “Jana, nilienda kwenye mkahawa wa bweni kula chakula cha mchana kama kawaida, na nikaona [ajali] kwenye TV. Nadhani nilishtuka sana nikaendelea kutazama habari hiyo huku mdomo wazi. Nilijisikia vibaya sana kuona ndege ikiwaka moto na magofu na wazima moto wakiitoa [miili]. Nina huzuni na uchungu kwamba raia wasio na hatia walilazimika kupoteza maisha hivi. “

Makumbusho yameanzishwa huko Muan, kusini-magharibi mwa nchi hiyo, ili familia za wahanga ziweze kutoa heshima zao. Mchongo wa upana wa mita 30 wenye umbo la jua utazinduliwa usiku wa manane karibu na Banda la Bosingak katikati mwa Seoul. Na sherehe ya Mwaka Mpya inapokaribia, matamasha ya hafla hiyo yote yamefutwa katika mji mkuu.

Jumatatu hii asubuhi, ndege nyingine ilipata hitilafu katika vifaa vyake vya kutua, kulingana na shirika la habari la Korea Kusini Yonhap. Shirika hilo linaripoti kuwa ni aina ya ndege hiyo hiyo, Boeing 737-800, kutoka kampuni ya Jeju Air, ambayo imekubwa na tatizo hilo. Ndege hiyo ililazimika kurudi nyuma.

Wizara ilituma wakaguzi wa usalama kwenye eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gimpo. Lakini hakuna uhusiano kati ya kesi hizo mbili umeanzishwa kutoka kwa chanzo cha kuaminika. Moja ya masanduku nyeusi ya ndege iliyoanguka imeharibiwa kulingana na mamlaka. Marekani inaweza kushiriki katika uchunguzi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment