Kifo cha Jimmy Carter: Biden atangaza maombolezo ya kitaifa Januari 9, 2025

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Taasisi yake ya Kituo cha Carter imesema rais huyo wa zamani amefariki akiwa nyumbani kwake mjini Plains, akiwa amezungukwa na familia yake.

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter (hapa alikuwa Ghana) alijitambulisha, na taasisi yake, Carter Center, baada ya kumalizika kwa muhula wake kwa safari zake nyingi nje ya nchi kwa ajili ya amani, demokrasia na maendeleo.
Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter (hapa alikuwa Ghana) alijitambulisha, na taasisi yake, Carter Center, baada ya kumalizika kwa muhula wake kwa safari zake nyingi nje ya nchi kwa ajili ya amani, demokrasia na maendeleo. The Carter Center/L. Gubb

Mdemocrat Carter, rais wa 39 wa Marekani, aliishi muda mrefu zaidi baada ya muhula wake madarakani kuliko rais mwingine yeyote wa nchi hiyo.

Carter alikuwa rais wa kwanza wa Marekani kuzaliwa katika hospitali, Oktoba 1, 1924 mjini Plains, jimboni Georgia. Mama yake alikuwa muuguzi na mmiliki wa duka la jumla. Baada ya maisha ya utotoni yaliyogubikwa na kipindi cha Mtikisiko Mkubwa kiuchumi, alijiunga na Chuo cha Jeshi la Wanamaji na akapendana na rafiki wa dada yake Rosalynn Smith. Walioana mwaka wa 1946 na wakaishi Pamoja kwa miaka 77, hadi Rosalynn alipofariki Novemba 2023 akiwa na umri wa miaka 96.

Wakati Carter alipoapishwa kuchukua madaraka kama rais wa Marekani Januari 20, 1977, aliahidi “serikali nzuri kama walivyo watu wake. “

Alikabiliana na kipindi cha miaka minne iliyokuwa na misukosuko. Kupanda kwa mfumuko wa bei na ongezeko la ukosefu wa ajira ambao uligubikwa na vipaumbele vya ndani katika utawala wake.

Alisifika kwa sera za mambo ya nje kwa mkataba wa amani kati ya Misri na Israel na mkataba wa Mfereji wa Panama.

Hata hivyo, mzozo wa mateka nchini Iran ulitawala miaka yake ya mwisho katika White House na kuchangia kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu wa 1980.

Jimmy Carter aliingia katika siasa katika miaka ya 1960, na kuhudumu kwa vipindi viwili kama mbunge wa Georgia kabla ya kuwa gavana wa 76 wa jimbo hilo kutoka mwaka 1971 mpaka 1975.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment