Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Rais wa Azerbaijani Ilham Aliev amebainisha Jumapili Desemba 29 kwamba ndege ya Shirika la ndege la Azerbaijan ambayo ilianguka siku ya Jumatano 25 huko Kazakhstan, na kuua watu 38, ililengwa na “kombora” kutoka Urusi, wakati chanzo cha tukio hilo ni urushaji wa kombora la kutungua ndege la Urusi linaonekana kuthibitishwa.
“Ukweli ni kwamba ndege ya kiraia ya Azerbaijani iliharibiwa kutoka nje katika ya anga ya Urusi … mkia wa ndege uliharibiwa vibaya na moto kutoka ardhini,” Ilham Aliev amesema katika mahojiano ya runinga, yaliyorushwa na shirika la habari la Azertag. Pia amesema ndege hiyo ilishindwa “kudhibitiwa” na uwezo wa kijeshi kutokana na hali iliyokuwepo.
Matoleo mbalimbali ya ukweli yaliyotolewa na Urusi baada ya ajali hiyo “inaonyesha wazi kwamba upande wa Urusi ulitaka kuficha jambo hilo. (…) Kukiri hatia (ya mtu), kuomba msamaha kwa wakati kwa Azerbaijani, ambayo inachukuliwa kuwa nchi rafiki, na kujulisha umma kuhusu hilo, hizi zote ni hatua na taratibu ambazo zinapaswa kuchukuliwa, amesema kwenye televisheni ya kitaifa.
Wataalamu wa anga wamesema kwamba huenda mfumo wa ulinzi wa anga wa Urusi ulikuwa chanzo cha ajali ya ndege ya Azerbaijan iliyotokea siku mbili kabla, ambayo ilisababisha vifo vya watu 38 na kuwajeruhi manusura wote 29.
Ndege ya Azerbaijani Airlines aina ya Embraer 190 ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Azerbaijan, Baku, kwenda Grozny, mji ulioko Kaskazini mwa Caucasus nchini Urusi, siku ya Jumatano ilipoelekezwa kwenye njia nyingine kwa sababu ambazo bado hazijafahamika na kuanguka wakati wa jaribio la kutua Aktau, Kazakhstan, baada ya kuruka mashariki kupitia Bahari ya Caspian.
Ajali hiyo ilitokea takriban kilomita 3 kutoka Aktau, ambapo picha za simu za mkononi zilizosambazwa mtandaoni ziliionyesha ikishuka kwa kasi kabla ya kuanguka na kulipuka kwa moto mkubwa. Picha nyingine zilionyesha sehemu ya nyuma ndege hiyo ikiwa imekatikia kwenye mabawa na ikiwa imelala juu chini kwenye nyasi.
Azerbaijani iliomboleza waathirika wa ajali hiyo Alhamisi kwa kushusha bendera nusu mlingoti kitaifa. Trafiki ilisimama saa sita mchana huku meli na treni zikilia king’ora kwa dakika ya ukimya kuwakumbuka waliofariki.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.