Israel: Familia za mateka zamtaka Donald Trump kuweka shinikizo kwa serikali ya Israel

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Familia za mateka zilmeandamana Jumamosi jioni katika miji kadhaa, na kumtaka rais mteule wa Marekani kumshinikiza Waziri Mkuu wa Israeli kwa makubaliano huko Gaza. Familia hizo zinamtaka Donald Trump kumshinikiza Benjamin Netanyahu kukubali makubaliano wakati ambapo mazungumzo kati ya Israel na Hamas yanaonekana kukwama tena.

Israel, Tel Aviv, Desemba 28, 2024: familia za mateka zinaandamana kwa ajili ya kuachiliwa kwa wapendwa wao. Wengi wanamtaka Rais Mteule Donald Trump kuishinikiza serikali ya Israel kudai mazungumzo na Hamas kuhusu Gaza.
Israel, Tel Aviv, Desemba 28, 2024: familia za mateka zinaandamana kwa ajili ya kuachiliwa kwa wapendwa wao. Wengi wanamtaka Rais Mteule Donald Trump kuishinikiza serikali ya Israel kudai mazungumzo na Hamas kuhusu Gaza. AP – Ariel Schalit

“Netanyahu anaendelea kuwa mhujumu mkuu wa makubaliano,” anasisitiza Einav Zangauker, mama wa Matan, mateka wa Hamas.

Hii ni wiki muhimu kwa hatima ya mateka. Na wapendwa wao wanatoa wito wa haraka, uliyoelekezwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli, lakini pia kwa Rais Mteule wa Marekani Donald Trump.

Yehuda Cohen ni babake Nimrod, 19, ambaye amezuiliwa huko Gaza tangu Oktoba 7, 2023. “Ninamwomba Rais Mteule Donald Trump asilegeze shinikizo lake kwa Mashariki ya Kati. Na Israel iko Mashariki ya Kati na hivyo hivyo Netanyahu… Ni lazima binafsi kumtishia Waziri Mkuu na kumwambia wazi: ikiwa hakuna makubaliano, atakuwa na matatizo.

Labda wewe ndiye wa mwisho ambaye unaweza kuweka shinikizo kwa Netanyahu, familia zinamwambia Donald Trump.

Ifat Kalderon, binamu wa Ofer, mateka , raia wa Ufransa mwenye asili ya Israel, anashambulia malengo ya mawaziri wa siasa kali za mrengo wa kulia wa muungano wa serikali. “Ben Gvir na Smotrich wanataka kujenga makazi huko Gaza kwenye migongo ya mateka. Netanyahu anashirikiana nao, na anafanya hivyo kinyume na matakwa ya watu. Benjamin Netanyahu na washirika wake wenye msimamo mkali wanawatoa mhanga raia na wanajeshi kwa udanganyifu wa kimasihi. “

Ofisi ya Waziri Mkuu imekanusha ripoti kwamba Israel na Hamas wanaweza kufikia makubaliano “ya kikomo” ya utekaji nyara kama ishara ya nia njema kabla ya kuanza kwa muhula wa pili wa Donald Trump.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment