India: Mahakama ya Juu yataka kusitisha mgomo wa kula wa kiongozi wa wakulima

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Tangu Novemba 26, mwanaharakati kutoka jimbo la Punjab, kitovu cha maandamano ya wakulima nchini India, hajala, kudai mapato bora kwa wakulima. Mahakama ya Juu inashtumu jimbo hili kwa kuruhusu hali kuzorota.

Polisi walirusha mabomu ya machozi kuwatawanya wakulima wanaoandamana karibu na mpaka wa Punjab-Haryana huko Shambhu, Desemba 8, 2024.
Polisi walirusha mabomu ya machozi kuwatawanya wakulima wanaoandamana karibu na mpaka wa Punjab-Haryana huko Shambhu, Desemba 8, 2024. © AP/Rajesh Sachar

Mnamo mwaka 2020 na 2021, makumi ya maelfu ya wakulima walikalia maeneo ya karibu ya New Delhi. Hali hii ilimlazimu Waziri Mkuu Narendra Modi kurudi nyuma juu ya ukombozi wa masoko ya kilimo. Lakini wakulima wengi huko Punjab – kikapu cha ngano nchini India – wanachukulia kupungua huku kuwa haitoshi.

Kwa zaidi ya mwezi mmoja, Jagjit Singh Dhaliwal amekuwa akifunga (kujizuia kula) kwenye mpaka kati ya Punjab na Haryana, ambapo serikali inajaribu kuzuia maandamano. Mfungo ambao ulichukua mkondo wa kisiasa wa kitaifa siku ya Jumamosi, Desemba 28, wakati Mahakama ya Juu ilipowataka viongozi wa eneo hilo kumhamisha hospitalini kabla ya Desemba 31, kutokana na hali yake mbaya ya kiafya.

Jagjit Singh Dhaliwal hali yake yakiafya imedorora

Jagjit Singh Dhaliwal anakataa kupelekwa popote, akisema yuko tayari kufa kwa ajili ya matakwa ya wakulima: dhamana ya bei ya chini inayopatikana ya ununuzi wa mazao yao.

Jimbo la Punjab linasema halina uwezo wa kumlazimisha, haswa kwa vile hema lake limezingirwa na wakulima wengi wanaolinda mgomo wake wa njaa. Mwezi huu wa Desemba, maandamano matatu ya wakulima waliokuwa wakisafiri kutoka Delhi yalizuiwa kwenye mpaka wa Haryana.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment