Visiwa vya Chagos: Washington yaingia katika mazungumzo kati ya Uingereza na Mauritius

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Katikati ya mazungumzo juu makubaliano kati ya London na Port Louis kuhusu uhuru wa Chagos, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amezungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Mauritius Navin Ramgoolam. Mazungumzo haya yasiyo ya kawaida yanasisitiza umuhimu wa kimkakati wa visiwa hivyo kwa Washington. 

Muonekano wa angani wa Diego Garcia, katika Bahari ya Hindi.
Muonekano wa angani wa Diego Garcia, katika Bahari ya Hindi. Pictures From History/Universal – Pictures from History

Iwapo London ilitambua mamlaka ya Mauritius juu ya visiwa vya Chagos mwezi Oktoba, masharti ya makubaliano hayo yanasalia kupingwa, hasa kuhusu kituo cha Marekani huko Diego Garcia. Mazungumzo yanashika kasi kabla ya Donald Trump kuchukuwa mamlaka ya nchi mnamo Januari 20.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alichagua kufanya mazungumzo kwa njia ya simu, badala ya njia ya jadi ya kidiplomasia, kumpongeza Waziri Mkuu mpya wa Mauritius. Ikiwa mazungumzo yalilenga rasmi kukaribisha ushindi wa Navin Ramgoolam katika uchaguzi wa wabunge mnamo Novemba 10, vyanzo vya ndani vinafichua kuwa swali la Chagos lilikuwa kiini cha mazungumzo.

Mnamo mwezi Oktoba mwaka huu, katika uamuzi wa kihistoria, London ilitambua uhuru wa Mauritius juu ya visiwa vya Chagos. Hii ni ndani ya mfumo wa makubaliano kimsingi juu ya mzozo huu wa eneo ambao umedumu kwa miaka 56.

Mradi huo, hata hivyo, ulitoa nafasi kwa Mauritius kuachia mamlaka yake juu ya Diego Garcia kwa Uingereza, ambapo moja ya kambi muhimu zaidi za jeshi la Marekani duniani iko.

Tangu kuingia madarakani, seŕikali ya Ramgoolam imeanza mazungumzo upya ya mkataba huu, unaozingatiwa kutopendelea maslahi ya Mauŕitius. Wiki hii, mbele ya wafuasi wake, Waziri Mkuu aliangazia tofauti zinazoendelea katika masharti ya makubaliano hayo, haswa kuhusu suala la uhuru wa sehemu ya Uingereza.

Mustakabali wa kambi ya kijeshi ya Marekani huko Diego Garcia ndio kiini cha mazungumzo. Mauritius haidai kufungwa kwa kambi hii, lakini inadai malipo ya kodi ya nyumba. Mazungumzo yanazidi kuongezeka huku Donald Trump akikaribia kushikilia mamlaka ya uongozi wa Marekani Januari 20.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment