ECOWAS na Nigeria zakanusha shutuma za kuhatarisha usalama wa Niger

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) siku ya Ijumaa, Desemba 27, imeitetea Nigeria, ambayo inashutumiwa na nchi jirani ya Niger kwa kuwa mwenyeji wa wanajeshi wa kigeni na kupanga njama za kuhatarisha usalama wa nchi hiyo. Nigeria, kwa upande wake, imekanusha moja kwa moja.

Mkuu wa Majeshi ya Nigeria, Christopher Musa, mjini Accra, Agosti 18, 2023.
Mkuu wa Majeshi ya Nigeria, Christopher Musa, mjini Accra, Agosti 18, 2023. © AFP – GERARD NARTEY

Katika mahojiano yaliyorushwa hewani siku ya Jumatano, Desemba 25, kiongozi wa kijeshi wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani, alishambulia ECOWAS, na kuthibitisha kwamba Ufaransa ilikuwa imeanzisha kambi kaskazini mwa Nigeria, ambapo itawapa silaha makundi ya kigaidi ili kuvuruga usalama katika upande mwingine wa mpaka.

Kutokana na shutuma hizi, ECOWAS imeonyesha uungwaji wake mkono kwa Nigeria. Katika taarifa, ECOWAS “inaonyesha wasiwasi wake mkubwa juu ya madai yaliyotolewa dhidi ya Nigeria na mataifa mengine wanachama (….) kwamba wanafadhili ugaidi.” “Kwa miaka mingi, Nigeria imeunga mkono amani,” imesema taarifa hii, ambayo imetaja “mafanikio ya hivi majuzi yaliyorekodiwa na Jeshi la Pamoja la Kimataifa (…) ambalo linaonyesha dhamira ya nchi hiyo kwa amani na usalama katika kanda yote. “

Nigeria yafutilia mbali shutma dhidi yake

Katika taarifa tofauti kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Alhamisi, Desemba 26, Waziri wa Habari wa Nigeria anasisitiza: nchi yake haina ushirikiano “na Ufaransa au nchi nyingine yoyote” ili kuhatarisha usalama wa Niger. Siku hiyo hiyo, mkuu wa jeshi la Nigeria, Jenerali Christopher Musa, alikanusha vikali madai haya wakati wa chakula cha mchana na wanajeshi walioko katika eneo la Sokoto, ambalo linashiriki mpaka na Niger.

“Mhalifu yeyote anayetumia ardhi ya Nigeria kushambulia majirani zetu ni adui wa Nigeria,” alitangaza kwa wanajeshi wake. “Sisi ni wamoja na majirani zetu na tutahakikisha kwamba vitisho kama hivyo havitumiki,” aliongeza.

Ujumbe ambao alikariri jioni hiyo hiyo kwenye televisheni ya taifa ya NTA, akithibitisha kwamba wasiwasi pekee wa nchi yake ni kulinda amani katika eneo hilo, na kuongeza: “Nilitembelea Niger ambako niliweza kujadili masuala haya yote na wakuu wa majeshi. Rais wetu alituamuru kuwahakikishia kwamba Nigeria haijawahi kuruhusu na kamwe haitaruhusu kambi yoyote ya kigeni kuanzishwa katika ardhi yake. Hatujawahi na hatutawahi. “

Jenerali huyo pia alisifu “uhusiano wa kipekee” kati ya nchi hizo mbili ambazo zinashiriki “mpaka wa kilomita 1,500”, “dini” na “utamaduni mmoja”.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment